Ijumaa 20 Februari 2026 - 00:58
Awamu mpya ya mapambano dhidi ya Uislamu; umuhimu wa mkakati wa kushambulia sambamba na mbinu ya kujihami/ Kutumwa wahubiri elfu 50 kote nchini Iran katika siku za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani/ Msisitiz

Hawza/ Ayatollah Alireza A‘raafi, Mkuu wa Hawza za Elimu ya Dini nchini Iran, katika kikao cha kirafiki na walimu, wahubiri na wanafunzi wa Hawza kilichofanyika katika Shule ya Madrasa ya Fayziya mjini Qom Iram, katika kuukaribia Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, alirejea hali nyeti ya sasa na uzoefu wake binafsi tangu kipindi cha Mapinduzi, na akasisitiza umuhimu wa kuutambua kwa usahihi uwanja wa mapambano ya kitamaduni, kuchukua mkakati wa kushambulia sambamba na mbinu za kujihami, pamoja na uwepo wa wanazuoni moja kwa moja na wenye athari katika ulinganiaji.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Kumbukumbu ya msimamo thabiti wa wanazuoni hukk Fayziya/ Maadui wajue kuwa wanazuoni ni watumishi wa watu, wako mstari wa mbele, wamesimama kwa ujasiri kamili bila woga kwenye dini ya Mwenyezi Mungu

Ayatollah A‘raafi mwanzoni mwa hotuba yake alikumbushia tukio la ujana wake akasema: Takribani miaka hamsini na moja iliyopita, siku ya kwanza nilipoingia Fayziya nikiwa kijana wa miaka kumi au kumi na moja, tulikumbana na tukio ambapo maafisa wa SAVAK walikuwa wamevamia Fayziya na wanafunzi walikuwa wamewazunguka kwa duara ili wasiruhusu tangazo la Imam (r.a.) liondolewe ubaoni. Kila mara maafisa wa SAVAK walipogeuka, wanafunzi waliwapigia makelele ya dhihaka, na waliporudi kuangalia, wote walitulia. Siku yetu ya kwanza Fayziya iliambatana na tukio hili la kuvutia sana.

Aliyataja maudhui haya kuwa ni alama ya utambulisho wa wanazuoni na akasisitiza: Taasisi ya Hawza na wanazuoni wanapaswa kusimama kwa ujasiri kamili na uthabiti mbele ya mawimbi yote ya misukosuko. Hii ndiyo asili ya wanazuoni. Maadui wanapaswa kujua kuwa wanazuoni ni watumishi wa watu, wako kazini, na kwa ujasiri kamili bila woga wamesimama katika dini ya Mwenyezi Mungu.

Mkuu wa Hawza za Elimu ya Dini aliendelea kwa kurejea kumbukumbu ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi katika miaka ya sitini (Hijria Shamsia) na kuongeza: Nakumbuka usiku mmoja katika Msikiti wa A‘dham, kabla ya kipindi cha urais wake, kulifanyika kikao cha mazungumzo na maswali na majibu, naye alisimama kwa muda wa saa tano au sita akijibu maswali. Usiku huo tulirejea nyumbani takribani saa sita usiku, hali hiyo imebakia daima katika kumbukumbu yangu.

Awamu mpya ya mapambano dhidi ya Uislamu

Ayatollah A‘raafi huku akisema kuwa leo maadui wameingia katika mapambano ya pande zote dhidi ya Uislamu na Mapinduzi ya Kiislamu, alibainisha: Yale yaliyotokea katika miaka miwili iliyopita ni awamu mpya ya mapambano dhidi ya Uislamu, maadili ya Kiungu na Mapinduzi ya Kiislamu.

Akirejea mikondo iliyodanganywa katika matukio ya hivi karibuni alisema: Hatupaswi kujipa matumaini ya kupita kiasi; katika anga ya mitandao ya kijamii na kupitia uzalishaji mwingi wa maudhui, mashambulizi mazito dhidi ya dini yameundwa.

Mkuu wa Hawza za Elimu ya Dini akasisitiza jukumu zito la wanafunzi na wanazuoni akasema: Sisi na nyinyi lazima tuwe askari uwanjani; hata kama ni kwa ajili ya kumuongoza mtu mmoja tu, tushuke uwanjani. Hata ulinganiaji kwa mtu mmoja tu tuuone kuwa ni jambo muhimu.

Mapambano magumu ya ustaarabu na umuhimu wa mkakati wa kushambulia

Ayatollah A‘raafi huku akisema kuwa jamii yetu ya ulinganiaji inapaswa kufahamu mapambano magumu ya ustaarabu ya leo, alifafanua: Tuko katikati ya uwanja mzito wa mapambano dhidi ya uvamizi wa utamaduni wa kimada wa Magharibi. Kushiriki katika uwanja huu kunahitaji elimu, maarifa, maadili, ikhlasi, uthabiti na subira, hekima na busara, pamoja na kuwajua maadui wanaoulenga Uislamu kwa fikra mbovu. Kutambua mapambano haya na kuelewa misingi na chimbuko la fikra ambazo Magharibi huzitumia kuishambulia Uislamu na dini, ni jambo muhimu sana.

Akiashiria msisitizo wa mara kwa mara wa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi alisema: Katika kukabiliana na mashambulizi ya shubha tuna misimamo miwili:

1. Msimamo wa kujihami ambao lazima uwepo; lazima tusikilize maneno ya adui, tuyafahamu na tuyajibu kwa mantiki sahihi.

2. Na msimamo wa kushambulia, wa kinadharia na wa kiutendaji. Msimamo wa kushambulia maana yake ni kuchota ukweli kutoka ndani ya Kitabu na Sunna, na kutoka katika tajriba ya Mapinduzi kuchambua mitazamo, kisha kushambulia ngome za adui. Hii ni sanaa kubwa ambayo imekuwa ikisisitizwa mara kwa mara.

Ulinganiaji unapaswa kuwa wa kielimu, wa kijamii na wa kimalezi

Mkuu wa Hawza za Elimu ya Dini akasisitiza umuhimu wa mabadiliko katika mtazamo wa suala la ulinganiaji, na akabainisha nukta muhimu zifuatazo:

1. Ulinganiaji wa kielimu

Alisema: Ulinganiaji wetu unapaswa kuwa wa kielimu na wenye msingi wa hoja thabiti. Ikiwa tunalingania katika masuala ya hukumu za kisheria, rejea yetu ni Fiqhi tajiri ya Uislamu na vitabu vinavyoaminika kama “Al-‘Urwah” na “At-Tahrir”. Ikiwa tunaingia katika masuala ya itikadi, misingi ya elimu ya kalamu na vitabu madhubuti kwa mtazamo wa wanakalamu na wanafalsafa mashuhuri kama Allamah Tabataba’i, Shahid Mutahhari, Ayatollah Misbah na Ayatollah Jawadi Amuli, lazima iwe ndio msingi wa kazi. Ikiwa tunaelekea katika riwaya, ni lazima tuwe wataalamu wa riwaya na tuvitambue ipasavyo vyanzo vya hadithi.

2. Ulinganiaji; roho na mhimili wa shughuli za Hawza

Akirejea kauli ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi, aliutaja ulinganiaji kuwa ni roho na mhimili wa kazi zote za Hawza, akasema: Hata katika uzalishaji wetu wa kielimu tunapaswa kuwa na mtazamo imara juu ya suala la ulinganiaji. Mikondo yote ya Hawza inapaswa kuwa na hisia na mwelekeo wa ulinganiaji na uwepo katika uwanja wake.

3. Kufunika mahitaji na hadhira zote

Alisema: Tuna ulinganiaji wa jumla na wa kitaalamu; wa jadi na wa kisasa. Taasisi zote za Hawza na mwili hai wa wanafunzi na wanazuoni wenye hamasa wanapaswa kugawanya kazi kwa namna ambayo vipengele vyote vya kazi vionekane; elimu ya shule, vyuo vikuu, taasisi mbalimbali, msikiti ambao uko kileleni mwa mambo, na nyanja nyinginezo.

4. Kubaki wa jamii na kuunda miduara ya kati

Alisisitiza kuwa ulinganiaji lazima ubaki wa kijamii na akasema: Mtumishi aliyefanikiwa ni yule anayeshuka uwanjani na ifikapo mwisho wa Ramadhani awe ameunda miduara kumi ya kati; awaandae wanafunzi wazuri, walimu, wakufunzi wa Basij, wafanyabiashara na wanafunzi wa vyuo kwa namna ambayo wao wenyewe wachukue jukumu la kuimarisha na kuendeleza ulinganiaji.

5. Uratibu wa taasisi za ulinganiaji

Akirejea wingi wa taasisi za ulinganiaji kama Awqaf, Ofisi ya Ulinganiaji, Shirika la Ulinganiaji, Ofisi ya Mwakilishi wa Uongozi katika Vyuo Vikuu na Vikosi vya Ulinzi, pamoja na Maimamu wa Swala za Ijumaa, alisema: Kuna takribani mikondo ishirini inayofanya kazi ya ulinganiaji. Lazima mikondo hii iratibiwe, na uratibu nje ya Hawza pia ni jambo muhimu linalopaswa kutekelezwa.

6. Thamani maradufu ya kijana muumini wa leo

Alisema: Kijana anayekuja leo msikitini, Basij na katika kazi ya dini, thamani yake ni kubwa zaidi kuliko yule kijana wa zama za Mapinduzi na Vita vya Kujihami aliyejitoa mhanga nafsi yake. Kwa nini? Kwa sababu sisi katika ujana wetu tulikumbana kila siku na kauli mbili au tatu, lakini leo kijana wetu yuko mbele ya maelfu ya nyimbo na sauti zisizo za Kiungu. Wanyang’anyi wengi wamemzunguka kijana wa leo.

7. Ulinganiaji wa kimalezi

Alisema: Ulinganiaji lazima uzingatie kwa pamoja njia za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja, za jadi na za kisasa. Asili katika ulinganiaji ni kuona kina cha uwasilishaji wa ujumbe. Neno ulinganiaji katika utamaduni wetu lina mizizi katika malezi, na malezi yamefichika ndani yake.

8. Kufunika ngazi mbalimbali za maarifa

Alibainisha: Ulinganiaji wetu lazima ufunike ngazi tofauti; kuanzia maarifa ya msingi ya Uislamu hadi masuala ya leo na Mapinduzi ya Kiislamu yanayotokana na upeo huo mpana.

Mabadiliko na mafanikio katika sekta ya ulinganiaji

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha