Kwa mujibu wa ripota wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatollah Makarim Shirazi aliwapongeza Waumini na Mashia wote katika siku hii ya kumbukumbu ya Utume wa Mtume Mkarimu (s.a.w.w) na katika Sherehe ya kuvishwa kilemba kwa Wanafunzi, iliyofanyika katika Mji wa Qom kwa kuhudhuriwa na watu mbalimbali na Maulamaa, ambapo aliposema: Kuhusu Mtume (s.a.w.w), Masuala muhimu yamejumuishwa katika maandiko ya Qur'an, moja wapo ni miujiza na namna ya kuamiliana na watu kwa tabia nzuri na kwa huruma na mapenzi. Watu wa Bara Arabu walikuwa dhidi ya kila mmoja wao na walikuwa katika migogoro kwa miaka mingi.
Qur'an inasema: "Mgogoro na mvutano huu ulikuwa namna hii kwamba hata ingelitokea ukagawanya mali yote ya ardhi kati yao, bado uadui huu (baina yao) usingelipungua".
Aliendelea kusema: Katika mgogoro / mzozo na mvutano huu, walikuwa wakiuana sana kiasi kwamba mpaka rangi ya mto ikabadilika kutoka na Damu za Maiti. Watu kama hao na maadui kamwe hawawezi kuunganishwa pamoja. Sasa hivi Duniani tunaona pia watu wanauana na kuna uadui mwingi ambao kamwe hauwezi kutatuliwa.
Lakini Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema, "Mtume wa Uislamu aliweza kujenga mafungamano, mapenzi na wema baina yao, na watu waliokuwa maadui na kuuana kwa miaka mingi, ujenzi wa mafungano na mapenzi na wema baina yao, uliweza kuondoa chuki hii baina yao." Hii ni moja ya sifa bora na mwenendo wake mzuri.
Marjii Taqlid huyu alisema: Mwenyezi Mungu alizileta pamoja nyoyo hizi kupitia Nabii / Mjumbe wake Muhammad (s.a.w.w).
Ni lazima tuzingatie jukumu la Mubalighina na Watu wa Kiroho (Wana Dini) katika kuunganisha mioyo ya Watu. Kati ya watu ulio nao, ongeza urafiki baina yao na punguza mizozo, migogoro, na ugomvi uliopo baina yao kwa kujenga urafiki na mshikamano baina yao. Kulingania mshikamano na upendo na kuunda mafungano baina ya watu ni suala muhimu katika jamii ya leo.
Maoni yako