Alhamisi 6 Februari 2025 - 20:56
Fiqh iko juu ya nyanja za Kisayansi na Maarifa za Seminari (Hawza) / Matumizi ya Teknolojia mpya ya Kisayansi ni muhimu kwa Wanafunzi na watafiti wote

Mkurugenzi huyo wa Seminari (Hawza) za nchi hiyo amesisitiza juu ya ulazima wa kuwa na mazingatio ya Wanafunzi na nafasi katika uandishi wa athari zinazoendana na mahitaji ya kila siku na mahitaji ya mfumo wa Kiislamu kwa kutumia mbinu za kina za Seminari (Hawza) na fani mpya na Teknolojia mpya za kiutafiti.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatollah Alireza Arafi, kabla ya Adhuhuri (saa sita mchana) leo hii, katika hafla ya kufunga Kongamano la Miaka 26 la Vitabu vya Hawza na Tamasha la Nane la Makala ya Kisayansi la Hawza lililofanyika katika Seminari ya Imam Kadhim (a.s) huko katika Mji wa Qom, alisema: 

Ayatollah al_Udhma Shabiri Zanjani anahesabiwa kuwa mmoja wa watu mashuhuri na nyota wanaong'aa wa Kisayansi ya Seminari (Hawza), na alikuwa chimbuko la kheri, baraka na neema kwa seminari kwa miongo mingi, ambapo alipewa heshima makhsusi katika mkutano huu.

Mkurugenzi wa Seminari (Hawza) nchini Iran aliongeza: Mkutano huu ni sherehe maalum ya makumi ya juhudi za bidii za Mwanazuoni huyo mkubwa wa Kishia. Vitabu vyake vya Nikah vyenye Juzuu 12 ni miongoni mwa vitabu muhimu vya Seminari. Alitoa baraka nyingi kwa jamii katika kilele cha juu cha (Sayansi ya) Fiqhi. Tunatumai kwamba juhudi zitafanywa kukusanya, kuhariri na kuchapa kazi / athari zake zote za Kifiqhi ili kazi / athari hizi zisajiriwe na kurekodiwa katika hazina kuu ya Seminari (Hawza). 
 
Ayatollah Arafi alisema: Hawza inapaswa kuwa na mitazamo miwili bora: Mtazamo wa kwanza, ni mtazamo wa kimsingi na wa kina na wa muda mrefu katika nyanja za Kisayansi na Maarifa ambapo Fiqhi iko kwenye kilele chake. Ni lazima tufuatilie maendeleo ya mipaka ya Kisayansi ya Fiqhi na Sayansi za Kiislamu kwa moyo wetu wote, na hakuna kitakachopaswa kuwa kisingizio cha kujiepusha na kurefusha mipaka ya Sayansi za Kiislamu. Fiqhi ya Jawaheri, Sayansi na Mafundisho ya Kiislamu yafuatwe kwa umakini na kina.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha