Alhamisi 6 Februari 2025 - 20:44
Pongezi maalum kwa miaka ya juhudi za Kisayansi za Ayatollah Mkuu Shobeiri Zanjani na Ayatollah Ray Shahri (r.a)

Katika Kongamano la 26 la Kitabu cha mwaka cha Hawza, Mamlaka ya Kisayansi iliwatunuku Ayatollah al_Udhma Shobeiri Zanjani na Hayati Ayatollah Ray Shahri.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Kitabu cha mwaka wa 26 na Tamasha la 8 la makala za Kisayansi za Seminari nchini; ilifanyika katika Seminari (Hawza) ya Imam Kadhim(a.s) kabla ya adhuhuri kwa kuhudhuriwa na watu Mashuhuri wa Seminari nchini Iran na nchi mbalimbali za nje zikiwemo Misri, Iraq n.k.

Katika hafla hii, Ayatollah Al_Udhma Shobeiri Zanjani alitunukiwa kwa miaka yake ya juhudi za Kisayansi (Kielimu) kama mhusika maalum wa Kisayansi (Kielimu) wa Mkutano wa 26 wa Kitabu cha Mwaka. Pia, Kitabu chake cha "Nikah" chenye Juzuu Kumi na mbili kilichaguliwa kama Kitabu bora zaidi cha mkutano huu.

Pia, Baraza la Kisayansi la 26 la Kisayansi lilianzisha Kitabu cha Mwaka wa Seminari (Hawza) kwa kutambua miaka 60 ya juhudi za Kisayansi, Ayatollah Ray Shahri kama Hadithi bora na Shakhsia wa Kisiasa wa Seminari (Hawza).

Katika Sherehe / Marasimu hii, Kazi zilizochaguliwa za Kisayansi za uwanja huo, pamoja na vitabu, nadharia na nakala za Kisayansi, zilithaminiwa.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha