Alhamisi 6 Februari 2025 - 07:17
Hebu tuimarishe uhusiano wetu na Hadhrat Waliyyul al_Asr (a.s) / Tujue thamani na nafasi ya mavazi ya kiroho

Hadhrat Ayatollah Nouri Hamedani amesema: Alisisitiza kuwa ni jambo la lazima kwa Mwanafunzi kuwa na maadili mema, ikhlasi, elimu na akili na akasema: Tujivunie kuwa askari wa Imam wa Zama (Mwenyezi Mungu aharakishe kudhihiri kwake) na tuimarishe uhusiano wetu pamoja naye.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, katika mnasaba wa sikukuu za Shaabaniyyah, ilifanyika Sherehe ya kuvalisha Kilemba kwa Wanafunzi wa Madrasat ya Kielimu ya Hojjatiyysh ya Qom mbele ya Ayatollah Nouri Hamedani pamoja na Shakhsia mbalimbali ndani ya Nyumba ya Mheshimiwa huyo (Ayatollah Udhma).

Marjii huyu wa Taqlid alichukulia jukumu la Viongozi wa Kiroho (Masheikh) kuwa ni jukumu zito sana katika wakati huu, na akanukuu Hadithi kutoka kwa Imamu Sadiq (amani iwe juu yake) kuhusiana na Mlango wa Hekima (Akili), na Ujinga (Ujahili) kutoka katika Kitabu cha Usul Kafi, na vile vile akataja aina za majukumu kutoka ndani ya Nahj al-Balaghah na akanukuu Barua ya 53 ya Hazrat Amir al-Muuminin (a.s) kwa Malik Ashtar na akasema:

Kwa kuzingatia uwepo wa Shubuhat (Ishkalat) mbalimbali katika Mitandao ya Kijamii, Wanafunzi ni lazima wawe na umahiri (ufahamu) kamili na Sahihi wa Qur'an na Hadithi.

Ayatollah Al_Udhma alieleza pia kuwa maadili mema, ikhlasi, elimu na akili ni muhimu zaidi kwa Mwanafunzi, na akaongeza: Hebu tujivunie kuwa maaskari wa Imam wa Zama (a.t.f.s) na tuimarishe uhusiano wetu pamoja naye.

Katika hafla hii, Wanafunzi walivishwa vilemba kupitia mkono wa Ayatollah Al_Udhma Nouri Hamedani.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha