Jumapili 2 Februari 2025 - 08:55
Mtazamo wa Fikra za Kiislamu na Tablighi za Kidini vinapaswa kuegemezwa kwenye Aya za Qur'an Tukufu na ufafanuzi unaotokana na Shule (Madrasat) ya Ahlul-Bayt (a.s)

Ayatollah Subhani amesema: Mhimili wa Fikra za Kiislamu na Tablighi za Kidini inatakiwa iwe ni kwa kutumia Aya za Qur'an Tukufu na ufafanuzi unaotokana na Madhehebu ya Ahlal-Bayt (a.s), hivyo watumishi mashuhuri Qur'an Tukufu, kwanza kabisa, wanaweza kujiimarisha kwa misingi ya Kisayansi za Qur'an, ili waweze kutatua mashaka / shubuhat kwa kurejelea Aya za Quran katika kila mjadala na hotuba inayokuja mbele yao.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Maandiko ya ujumbe wa Hazrat Ayatollah Jafar Subhani kwa Baraza la Wahudumu wa Qur'an Tukufu kote nchini, yalisomwa na Morteza Najafi Qudsi, mmoja wa Wahudumu wa Qur'an Tukufu kutokea katika Mji wa Mashhad, leo hii, Ijumaa 31 / 01 / 2025, na maandiko hayo kama ifuatavyo:

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu.

"Walipotumwa Mitume ulimwenguni, Mitume miongoni mwao waliwasomea Aya na Yazkihim, na wakawafundisha Kitabu na hikima, mmoja wao kabla yangu nilichanganyikiwa."

Kufanyika Mkutano Mkuu na Mkutano wa Watumishi / Wahudumu wa Qur'an Tukufu kutoka kote nchini katika Mji wa Mashhad Tukufu na Karibu na Haram Tukufu ya Imam wa Nane Ali Ibn Musa al-Ridha (a.s) na katika siku za neema ya Bi'itha / Utume wa Mtume wa Uislamu (s.a.w.w), ni fursa nzuri kwa Watumishi / Wahudumu wa Qur'an nchini kujumuika pamoja na kufikiri juu ya masuluhisho ya ukuaji na uboreshaji wa Utamaduni wa Kidini na wa Qur'an katika Jamii.

Kusudio kuu la Bi'itha / Utume wa Mtume wa Mwisho (s.a.w.w) lilikuwa ni kusoma Aya za Mwenyezi Mungu na kufafanua kanuni za Sharia ya Kiislamu, kuwalea Waislamu, na kufundisha na kujifunza Qur'an na Hekima ya Mwenyezi Mungu.

Harakati ya Utume / Bi'itha ilianza kwa Aya za Qur'an Tukufu, na katika kipindi cha miaka 23 ya Utume wake (s.a.w.w), jumla ya Aya 6236 ziliteremshwa kwake na Malaika Jibril Mwaminifu (Amani iwe juu yake), ambaye ni Malaika wa Wahyi wa Mwenyezi Mungu kwa Mtume wake (s.a.w.w), pamoja na juhudi zake zote bila kuchoka na ugumu alioweza kuustahimili katika muda huu mrefu kwa ajili ya kueleza Aya za Mwenyezi Mungu na kuwatakasa watu na jamii ya Wanadamu (kupitia mafunzo yake).

Ni wazi kabisa kwamba mhimili wa Fikra za Kiislamu na Tablighi za Kidini unapaswa kuegemezwa juu ya Aya za Qur'an Tukufu na ufafanuzi uliochukuliwa kutoka Shule / Madrasat ya Ahlul-Bayt (a.s), hivyo Watumishi / Wahudumu Mashuhuri wa Qur'an Tukufu wanapaswa kwanza kabisa wajitie nguvu katika misingi yao ya kisayansi ya Qur'an katika kila Mijadala na Hotuba zinazojitokeza mbele yao, ambapo itawasaidia waweze kutatua mashaka / shubuhat kwa kurejelea Aya hizo za Qur'an Tukufu.

Lakini Utume uliotukuka wa Mtume (saww) haukuishia tu kwenye usomaji wa Aya, bali pia ulikuwa ni juhudi kubwa ya kukuza na kukamilisha maadili mema.

Mwalimu wa Qur'an lazima aikuze nafsi yake katika nuru ya kimungu ya Qur'an Tukufu na ajiendeleze mwenyewe, na ikiwa mtu hatokuwa na Taq'wa na Mcha Mungu, basi huyo hawezi kudai kuwa mhudumu wa Qur'an Tukufu.

Uteuzi wa kila mwaka wa watu wachache kama watumishi / Wahudumu wa Qur'an Tukufu unatoa fursa nzuri kwa wanaharakati wa Qur'an kutilia maanani zaidi uimarishaji na upanuzi wa shughuli za Qur'an.

Ushirikiano wa Watumishi / Wahudumu wa Qur'an nchini unaweza kuwa kama mti mzuri ambao mizizi yake imeimarika / ni thabiti na matawi yake yameelekea juu angani.

Heshima ya kuwa mhudumu wa Qur'an na Itrah wa Mtume (s.a.w.w) ambapo ni Vitu viwili visivyotenganishwa, iwaongezee mazingatio na ari ya kutumikia zaidi katika uwanja wa Neno la Mwenyezi Mungu.Na Qur'an Tukufu daima itakuwa imejaa Kheri, Neema na Baraka kwa watu na nchi kwa ujumla, na hiyo ndio fadhila kubwa.

Jaafar Subhani

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha