Jumatano 29 Januari 2025 - 16:28
Seminari / Hawza ya Kielimu ni mahali pa kujitolea na mapambano

Sherehe ya kuvalisha vilemba kwa Wanafunzi kadhaa wa masomo ya kidini wa Seminari (Hawzat) ya Iravan Mjini Tehran katika Mnasaba wa Mab'athi / Kutumwa kwa Mtume Muhammad al_Mustafa (Rehma na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na Aali zake), ambazo zimefanyika mbele ya Ayatollah A'rafi, Mkurugenzi wa Seminari zote nchini Iran, Hojjat al-Islam wal_Muslimeen Rahimi Sadegh, Mkurugenzi wa Seminari ya Mkoa wa Tehran, Hojat al-Islam wal_Muslimeen Shabastari msimamizi wa Seminari ya Teolojia ya Iravan, Walimu na Wanafunzi wa masomo ya kidini, walihudhuria katika Sherehe hiyo ilifanyika kwa kuanza na kisomo cha baadhi ya Aya za Qur'an Tukufu na kusomwa kwa kaswida moja ya sifa njema kupitia kwa mmoja wanafunzi katika Seminari hii.

Kwa mujibu wa ripota wa Shirika la Habari la Hawzat, katika hafla hii, Ayatollah A'rafi alitoa ufafanuzi kuhusu sehemu ya Dua za Mwezi wa Rajab na kusema: Dua za Mwezi Mtukufu wa Rajab, zinashirikiana katika lengo moja, lakini zina madhumuni zisizo za kawaida. Miezi ya Rajab, Sha'ban, na Ramadhani ni tofauti kabisa na nyakati zingine, za mchana na usiku, na kwa mujibu wa ushahidi tunaofaidika nao, vipindi vya nyakati ni tofauti kwa mujibu wa Ushahidi wa Ki_Mungu na Kiroho.

Baadhi ya wazee wamesema nao wanasema kutoka kwa Wazee (Wahenga) kuwa nyakati zote ni sawa, ispokuwa zinakuwa tofauti kwa sababu ya matukio tofauti tofauti, Zama za muda zinafanana na ziko sawa, lakini zinatofautiana kutokana na matukio tofauti tofauti.

Aliendelea kusema: Nyakati ni tofauti na ufalme wa nyakati hizi una utofauti kwa dalili yoyote ile.

Miezi ya Rajab, Shaban na Ramadhani ina Nuru na Mwangaza wa juu zaidi. Maana ya Hotuba hii sio mjadala wa kimwili (kifizikia) juu ya nyakati au wakati wa Kalenda. Kwa sababu milki hii ya nyakati, sura hii ya nyakati, ni chombo tu ambacho kwa sasa (ndani yake) ni Mwezi wa kwanza wa Rajab, ambapo watu Bilioni nane Duniani leo hii tayari wameingia katika Mwezi huu, ambao ni kawaida kwa kila mtu, kwa maana kila mtu anaingia katika wakati wa Rajab, Sha'ban na Ramadhani, lakini hii Sha'ban Na Ramadhani na Rajab ni Miezi ambayo ina ufalme wa mbinguni na wa ghaibu ambao si kila mtu anaweza kuingia katika ufalme huo.

Kuingia katika Miezi ya Rajab, Sha'ban na Ramadhani ni uingiaji makhsusi na umetengwa kuwa makhsusi kwa wale tu wanaostahiki Miezi hii.

Akaongeza: "Watu Bilioni themanini Duniani sio kwamba wanatakiwa kuelewa ukweli / uhakika wa kuandama kwa Mwezi wa Ramadhani kwa kuona Mwezi Mpevu wa Ramadhani, lakini hawawezi kamwe wote kufikia hatua ya uhakika wa Lailat Al-Qadri." 

Laylat al-Qadri na Ramadhani, Sha'ban na Rajab ni (Miezi) ina hadhi maalum ambayo haipatikani kwa watu wote Duniani; na haya ni masuala ya msingi yaliyopo katika Shari'ah.

Sisi na ninyi, ambao mmeingia katika Seminari (Hawzat), lazima tufungue milango hii, tupande vilele hivi, na mojawapo ya njia ni kuelewa uhakika / ukweli wa kifalme wa nyakati hizi za kiupendeleo na zinazostawi.

Mkurugenzi wa Seminari (Hawzat) zote nchini alishauri kusoma kitabu cha al-Muraqabaat cha Hayati Sheikh Jawad Malaki Tabrizi. Kitabu hiki na programu iliyowasilishwa katika Kitabu hiki ni dirisha linaloongoza kwenye upeo wa ukweli / uhakika wa Rajab, Sha'ban na Ramadhani na kinatufungulia milango hiyo.

Wapendwa ambao leo watavaa nguo zinazoashiria maadili ya kimungu na ya kidini lazima waelewe ukweli huu na waelewe starehe hizi, na ufahamu huu unahitaji kazi.

Mjumbe wa Baraza Kuu la Seminari aliendelea kwa kueleza sifa za Miezi ya Rajab na Sha'ban: Miezi ya Rajab na Sha'ban ina maudhui na pia miezi hii yenyewe kama ilivyo ni nyakati zinazostawi na ambazo pia ni Miezi yenye kuonyesha njia na pia ni hatua zinazoongoza, ambapo huwaongoza watu wanaolekea kuelekea kwenye Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na hatimaye kufika kwenye kilele cha juu na cha mwisho kabisa cha Laylatul_Qadri.

Matumizi ya chombo hiki (Mwezi wa Rajab) pia yanahitaji Mwongozo na Kanuni. Dua na ibada za Mwezi wa Rajab ni miongoni mwa Kanuni zinazoweza kuwekwa kwenye njia hii kuu na njia ya nuru ili kupatikana kwa maelewano ya dhati kati ya nafsi zetu na uhakika wa Mwezi wa Rajab, Sha'ban na Ramadhani.

Mkurugenzi wa Seminari nchini alisisitiza kwamba Seminari zinapaswa kuwa hai kwa mtazamo wa kijihadi (mapambano): Ikiwa utakuza sifa nzuri moyoni mwako, na ukijihandisi na kujisimamia na kujenga vizuri muundo wa ndani yako ipasavyo, matokeo yake yatakuwa ni wewe kutenda mambo makubwa (mambo makubwa yatachemka) ndani ya moyo wako. 

Wale ambao wameingia katika Hawzat / Seminari, wanapaswa kujiandaa katika hali zote za shida na ugumu (kujifunga kibwebwe) na kufanya kazi kama vile mpiganaji wa jihadi ili kuwaongoza watu na kuendeleza mafundisho ya Mwenyezi Mungu.

Ikiwa mtu amekuja katika eneo hilo la Hawzat / Seminari ya Kidini kwa ajili ya kupata raha, faraja na kupumzika tu, huyo inapaswa kuambiwa kwamba amekuja kwenye njia hiyo kimakosa. Seminari / Hawzat ni mahali pa kujitolea na mapambano.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha