Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawzat, Hojjatul-Islam wal-Muslimin Hamid Maliki, Naibu Mkurugenzi wa Seminari (Hawzat) ya Qom, katika mkutano wa wajumbe wa kongamano la kumbukumbu ya Allamah Bahabadi, huku akishukuru juhudi zilizofanywa kumtambulisha Mwanazuoni huyo mkubwa wa Kishia, alitangaza utayarifu wa Seminari (Hawzat) ya Kielimu ya Qom katika kuunga mkono kongamano hili.
Akiashiria umuhimu wa kuarifisha shakhsia wenye ushawishi kwa kizazi kipya, alikosoa ukosefu wa juhudi katika uwanja huu na kusema: Mataifa mengine yanaunda hadithi (hikaya au historia) kutokana na haiba isiyokuwepo ya Shakhsia za watu wao wenyewe, lakini kwa bahati mbaya, sisi hatufanyi juhudi vya kutosha katika kuwatambulisha wanafikra (na wanazuoni) wetu kwa watu wa jamii ya kisasa.
Hojjat-ul-Islam wal-Muslimin Maliki alitaja ufufuaji wa athari na kuwakumbuka (kuwaenzi) Wanazuoni wa Shia kuwa ni jambo la lazima na akasisitiza:
Hili linahitaji uwekezaji na msaada katika kutoa rasilimali. Katika uwanja wa kuwatambulisha wanavyuoni wa Shia, tunapaswa kuzingatia zaidi jambo hilo. Wanafunzi wachanga wanahitaji kujua athari za kisayansi (kielimu) na jihadi za Wanafikra mbalimbali wa Hawzat.
Maoni yako