Kulingana na Shirika la Habari la Hawzat, Mkutano wa Kisayansi wenye anuani "Ikiwa Masih / Kristo angekuwa kati yetu..." na mada ya kibao chenye manukuu ya kauli za Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu yasemayo: "Ikiwa Masih / Kristo angekuwa miongoni mwetu...", ambao ulifanyika baada ya Hojat al-Islam wal-Muslimeen Mohammad Hussein Mokhtari, Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kuhudhuria katika Mkutano wa ana kwa ana na Papa Francis huko Vatican mnamo Januari 2, 2025 na kuwasilishwa ujumbe huo kwake.
Mkutano huu ulifanyika kwa kuhudhuriwa na kikundi cha Wanafunzi na Maprofesa wa Seminari (Hawzat) ya Qom kutoka Taasisi ya Utafiti ya Kimataifa ya Ar'wat Al-Wuthqa kwa ushirikiano na Taasisi ya Utafiti wa Kisayansi ya Kitamaduni ya Mapinduzi ya Kiislamu katika Mji wa Qom.
Hojjat al-Islam wal-Muslimeen Mohsen Qanbari, Makamu wa Rais wa Mawasiliano na Masuala ya Kimataifa wa Jumuiya ya Al-Mustafa, Dk. Kamal Akbari, Mkuu wa Kitivo cha Dini na Vyombo vya Habari, na Dk. Eliche Mijano, Mtafiti na Mwandishi kutoka Italia, walichunguza na kufafanua uteuzi wa kauli za Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kuhusu Yesu Kristo kwa Papa Francis iliyowasilishwa kwake na Ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Vatican.
Mwanzoni mwa Mkutano huu, Hojjat al-Islam wal-Muslimeen Jalal Iraqi, Mtafiti wa Taasisi ya Utafiti ya Kimataifa ya Ur'wat Al-Wuthqa na Katibu wa Mkutano huo, alipokuwa akijadili na kueleza Falsafa ya kufanya Mkutano huu na kusisitiza haja ya kuwepo kwa mazungumzo ya kidini ili kujibu mahitaji ya ubinadamu wa leo na ili kuweka amani na utulivu Duniani kote; na hatimaye kuelekea kwenye furaha ya Mwanadamu, ambapo maandishi ya kibao hicho yalisomeka hivi: "Ikiwa Yesu Kristo (a.s) angekuwa baina yetu".
Ujumbe wa Umoja na Uadilifu katika mafundisho ya Yesu Kristo (a.s) kwa mtazamo wa Qur'an na Hadith: Katika muendelezo wa Hojjat al-Islam wal-Muslimeen Qanbari, Makamu wa Rais wa mawasiliano na masuala ya kimataifa wa jumuiya ya Al-Mustafa ameashiria ufafanuzi wa umoja na uadilifu katika mafundisho ya Yesu Kristo (a.s) na kusema: Katika mkutano huu, itachunguzwa nafasi ya Yesu Kristo (amani iwe juu yake) katika Qur'an na Hadithi za Kiislamu.
Akirejelea Aya za Qur'an Tukufu na maneno ya Imamu Reza (amani iwe juu yake), Isa / Yesu Kristo (a.s) akiwa kama Neno la Mwenyezi Mungu na Mtume wa Mwenyezi Mungu, aliweka mbele katika majukumu yake ya kufikisha ujumbe suala la vita dhidi ya dhulma na ufisadi na kufanya juhudi za kueneza uadilifu na rehema.
Mafundisho haya ni mafunzo muhimu sio tu kwa Wakristo, bali kwa Wanadamu wote, haswa Waislamu. Leo, ni jukumu letu, kwa kuchochewa na mafundisho haya, kuratibu katika kuunda utaratibu wa ulimwengu unaozingatia maadili ya kibinadamu na maadili na kuimarisha umoja na ushirikiano kati ya dini mbalimbali. Natumai ujumbe huu unaweza kuwa hatua ya kufikia Haki na Amani Duniani.
Nafasi / Jukumu la Diplomasia ya Kitamaduni na vyombo vya Habari katika kukuza maadili ya Kibinadamu na amani ya ulimwengu: Kisha Dk. Kamal Akbari, Mkuu wa Kitivo cha Dini na Vyombo vya Habari wa Shirika la Utangazaji; Amesisitiza umuhimu wa ujumbe wa Kiongozi Muadhamu kwa Baba Mtakatifu Francisko na kusema:
Ujumbe huu unatumika kama daraja la kuimarisha uhusiano wa kimataifa na wa kidini hasa katika Ulimwengu wa Kikristo.
Diplomasia ya Kitamaduni na vyombo vya Habari vinaweza kusaidia kujenga maelewano na kupigana dhidi ya mawazo yenye msimamo mkali kwa kukuza maadili ya kibinadamu na maadili.
Pia walisisitiza nafasi ya vyombo vya Habari katika kuakisi hali halisi ya Binadamu na kusaidia wanyonge, hasa katika machafuko kama ya Gaza Kama Kristo angekuwa miongoni mwetu leo hii, angevitaka vyombo vya habari kuwa chombo cha kuhudumia ukweli, haki na amani (Duniani).
Mambo ya kushirikiana baina ya Uislamu na Ukristo: Dk. Aliche Mijano alitoa hotuba yake chini ya kichwa cha Habari: "Ujumbe wa umoja na ushirikiano kati ya Dini mbalimbali; Iliakisi mawazo ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu kuhusu Yesu Kristo (a.s).
Mtafiti huyu wa Kiitaliano akiushukuru Ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Vatican katika kuwasilisha ujumbe huu kwa Papa Francisco, amechunguza ujumbe wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatollah Khamenei kuhusu Yesu Kristo (a.s) na kuongeza:
Ujumbe huu unasisitiza umuhimu wa Yesu (a.s) katika Qur'an na Uislamu unasisitiza na kumtambulisha kama Nabii mtenda miujiza. Ujumbe huu unaonyesha hali ya kawaida ya Uislamu na Ukristo katika kumheshimu Yesu (amani iwe juu yake) na kujaribu kuunda amani na uadilifu duniani.
Amesema: Katika ujumbe huo Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu anazingatia kuwa mapambano dhidi ya dhulma na ufisadi ni miongoni mwa mafundisho makuu ya Yesu (amani iwe juu yake) na anatumai kuwa Waislamu na Wakristo watapata kuishi pamoja na kushirikiana kwa amani kwa kuchochewa na mafundisho hayo. Ujumbe huu pia unasisitiza ulazima wa mazungumzo baina ya Dini mbalimbali na kuimarisha hali ya kuheshimiana ili kuunda ulimwengu usio na vurugu na uliojaa amani.
Maoni yako