Jumapili 13 Aprili 2025 - 18:42
Bodi ya Raisi wa majmah-Mudarrisina yakutana na Maraji wa Najafu

Bodi ya Raisi wa Jumuiya ya Jaamiat-Mudarrisin ya Hawza ya Qom katika safari yake ya kwenda Najafu Ashraf ilikutana na baadhi ya maulamaa na wanazuoni, na walifanya mazungumzo kuhusu kuimarisha hawza, umoja wa Kiislamu, na uungaji mkono mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu.

Kwa mujibu wa idara ya habari za kimataifa ya Shirika la Habari la Hawza, Uongozi wabodi hiyo, ukiwa na rais na katibu wa baraza hilo, ulikutana na kufanya mazungumzo na Hadhrat Ayatollah Bashir Najafi, Wa’idh Sabzawari, Husseini (mwakilishi wa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi katika Iraq), Ya’qubi, na Sheikh Muhammad Sanad katika mji mtukufu wa Najafu Ashraf.

Malengo ya safari na utambulisho wa Jumuiya ya Jamiat-Mudarrisin

Hujjatul Islam wal Muslimin Sulaimani Ardehali, rais wa Jumuiya hiyo, katika mkutano huyo alitoa utambulisho mfupi wa taasisi hiyo na kueleza malengo ya safari hiyo. Akitaja nafasi ya jumuiya hiyo kama urithi wa Imam Khomeini (r.a) na ambayo imekuwa likisisitizwa na Kiongozi Mkuu, alieleza kuwa safari hiyo ni fursa ya kufanya ziara katika maeneo matukufu na kuimarisha uhusiano na maulamaa wa Najafu.

Sulaimani alisisitiza umuhimu wa ushirikiano endelevu kati ya walimu wa Qom na Najafu kwa ajili ya kusukuma mbele malengo ya Uislamu halisi, kuimarisha mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu, na kuwa macho dhidi ya njama za maadui. Pia aliwataka maulamaa na wanazuoni kutumia uwezo wa kielimu na kimalezi wa Jumuiya hiyo.

Maneno ya Ayatollah Bashir Najafi katika mkutano huo wa pamoja na ujumbe kutoka Qom

Hadhrat Ayatollah Bashir Najafi alisisitiza haja ya usimamizi wa karibu juu ya masomo na walimu wa hawza, na akaeleza: “Mpangilio na kanuni za kiutawala katika Najafu hazikuwepo tangu mwanzo, lakini Qom, kwa kuwa kuna serikali na mfumo, ni lazima kuwe na usimamizi na sheria.”

Alisisitiza kwamba, uhuru wa hawza unamaanisha kuwa serikali hazipaswi kuamrisha au kukataza ndani ya hawza, ili fikra na tafakuri za maulamaa zisipate hitilafu. Uhuru huu ni muhimu ili maulamaa waweze kutoa uongozi na kufanya istinbati kwa uhuru.

Hadhrat Ayatollah Bashir Najafi, pia alisisitiza umuhimu wa mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu na akatahadharisha: “Iwapo mfumo wa Iran utapata madhara, basi hata hawza za Najafu zitatetereka.”

Alisisitiza umuhimu wa kumuelekea Amirul Mu’uminin Ali (a.s.) na akasema: “Tusife ila kwa mapenzi na upendo juu ya Ali (a.s.).”

Ayatollah Najafii, akirejea hadithi ya “زر فانصرف” kuhusu ziara ya Imamu Hussein (a.s.), alieleza kuwa tamko hili linaonesha falsafa ya kina ambayo haikusudii kupunguza uzito wa msiba wa Imamu Hussein (a.s.), bali inalenga kudumisha upya wa huzuni na uhusiano wa moyo na msiba huo mkubwa.

Maneno ya Ayatollah Wa’idh Sabzawari katika kikao hicho

Ayatollah Wa’idh Sabzawari katika kikao hicho alisisitiza haja ya kuhifadhi hali ya kimaana ya hawza na kushikamana na Ahlul Bayt (a.s.), na akasema: “Najafu na Karbala vina nafasi ya pekee katika kujibiwa dua, na ni lazima tuhifadhi fadhila hii.”

Aliendelea kusema: “Katika riwaya imeelezwa kuwa dua chini ya kuba ya Imamu Hussein (a.s.) hujibiwa. Pia, katika riwaya nyingine imeelezwa kuwa dua mbele ya kaburi la Imam Ali (a.s.) hujibiwa, yaani Najafu. Na ikiwa ‘Najafu’ itachukuliwa kwa maana ya jumla, inaweza hata kuhusisha Karbala na eneo kubwa zaidi.”

Alisema kuwa, sisi ni wanyonge na hatuwezi chochote, lakini Imam Ali (a.s.) anatuwezesha, na tunapaswa kuomba uwezo huo kutoka kwake kwa kutawassal. Pia, tunapaswa kupata ilhamu kutoka kwa maulamaa wakubwa waliozikwa katika haramu yake.

Ayatollah Wa’idh alisisitiza kuwa kuamrisha mema na kukataza mabaya nchini Iran hakupaswi kudhoofishwa.

Aliendelea kusema kuwa ikiwa mfumo wa Iran utapata madhara, basi sote tutadhurika. Hivyo basi, ni lazima kulinda mfumo huo dhidi ya tishio lolote lile.

Ayatollah Wa’idh Sabzawari katika hitimisho alionya kuwa: “Tusiruhusu mabadiliko ya idadi ya watu kuwa dhidi ya Mashia, na Iran kugeuzwa kuwa uwanja wa dola ya Kisunni.”

Hitimisho la safari na ujumbe wa maulamaa

Katika hitimisho la kikao hichi, maulamaa na wanazuoni wa Najafu Ashraf, huku wakitoa pongezi kwa nafasi ya Jumuiya ya Jamiat-Mudarrisin, walisisitiza juu ya umoja wa hawza na uungaji mkono mfumo wa kiislamu. Pia waliiomba bodi kutoka Qom kuwafikishia walimu na wanafunzi wa hawza salamu zao.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha