Jumamosi 24 Mei 2025 - 20:56
Kwa mara nyengine tena Mahafali kubwa ya kimataifa ya Qur'ani yafanyika Tanzania

Hawza/ Mahafali kubwa ya Qur'ani ya kimataifa imefanyika Tanzania, huku maelfu ya waumini wakimiminika kushuhudia mahafali hiyo.

Shirika la Habari la Hawza - Nchi ya Tanzania imeshuhudia tena Mahafali kubwa na ya kipekee ya Qur'ani iliyofanyika katika jiji la Tanga nchini humo. Mahafali hiyo ambayo ilibeba nyuso tofauti kutoka ndani na nje ya nchi ilirindima katika viwanja vya Mkwakwani leo hii tareh 24/5/2025, huku maelfu ya wananchi kutoka mikoa mbalimbali wakiweza kubudhuria na kushiriki vyema katika kongamano hilo.

Kwa mara nyengine tena Mahafali kubwa ya kimataifa ya Qur'ani yafanyika Tanzania

Baadhi ya viongozi mbali mbali wa kidini wakiongozwa na Sheikh mkuu wa jumuiya ya Shia Tanzania (TIC), wakifuatilia kwa ukaribu mashindano hayo

Mahafali hiyo ambayo imeandaliwa vyema chini ya usimamizi wa chuo cha Almustafa, kichopo nchini Tanzania kwa kushirikiana na Baraza kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Kituo cha utamaduni cha Irani pamoja na Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT), ilifanyika leo hii huku umati mkubwa wa watu waliojitokeza kushuhudia umahiri wa wasomi wa Qur'ani kutoka nadani na nje ya nchi wakionesha ufundi na uhodari walio nao.

Kwa mara nyengine tena Mahafali kubwa ya kimataifa ya Qur'ani yafanyika Tanzania

Wakina Mama pia nao hawakuwa nyuma katika kushiriki kwenye Mahafali hii kubwa ya Qur'ani 

Viongozi mabali mbali wa kiserekali na wa kidini waliweza kushiriki vyema kwenye mahafali hiyo, huku mgeni rasmi akiwa ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt. Batilda Buriani, ambae kando na kuhudhuria kwenye mahafali hiyo, alitoa pongezi zake za dhati kwa waandaaji wa kongamano hilo kwani ni moja wapo ya njia zinazo onesha umoja, ushirikiaano na mafungamano katika jamii. Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shia Ithnaasharia Tanzania (TIC), Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT) Sheikh Alhadi Mussa, Mkurugenzi wa kituo cha utamaduni cha Wairani nchini Tanzani pamoja na msimamizi mkuu wa chuo cha Almustafa Tanzania, Dkt. Ali Taqavi.

Mwisho wa mahafali hiyo uongozi wa juu wa chuo cha Almustafa nchini Tanzania, ulitoa pongezi na shukrani za dhati kwa wahudhuriaji wote ambao walijitolea kwa hali na mali ili waweze kushiriki vyema katika mahafali hiyo.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha