Jumanne 27 Mei 2025 - 14:16
Ukuaji na Maendeleo ya chombo cha habari cha hawza katika Miaka mia moja ya hivi karibuni

Hawza/ Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya za Kitaaluma za Hawza, huku akieleza nafasi ya kimaendelea ya hawza katika kuanzisha na kuendeleza taasisi za vyombo vya habari, amezitaja juhudi za wanazuoni wa dini katika kuzalisha maarifa ya dini kwa kutumia njia ya vyombo vya habari, kuanzisha taasisi na kujenga mijadala katika uwanja wa vyombo vya habari kuwa ni jambo lisiloweza kupuuzwa.

Shirika la Habari la Hawza - Hojjatul Islam wal Muslimin Muhammad Reza Barte, kutokana  a mnasaba wa maadhimisho ya miaka mia moja tangu kuanzishwa upya kwa Hawza ya Qom, katika mahojiano na mwandishi wa Shirika la Habari la Hawza, amesema: "Kuzungumzia mafanikio ya vyombo vya habari vya vyuo vya hawza, kunahitaji fursa kubwa na ya kina, hata hivyo katika kipindi hiki cha miaka mia moja iliyopita, tunaweza kugusia baadhi ya mambo muhimu."

Ameongeza kwa kusema: Hawza ni miongoni mwa taasisi za mwanzo kabisa za kitamaduni nchini ambazo zimekabiliana na aina mpya za vyombo vya habari; vyombo vya habari ambavyo mwanzoni vilijitokeza kwa sura ya machapisho, kisha ikawa redio na vyombo vya sauti, baadaye televisheni, na hatimaye ikafikia katika uwanja mpana wa mitandao ya kidijitali."

Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya za Kitaaluma za Hawza ameendelea kusema: "Jambo la kuvutia ni kwamba wanazuoni wa dini ambao katika matumizi ya mali ya umma (baitul maal) wanachukua tahadhari na uangalifu wa hali ya juu, katika miaka ya mwanzo ya karne hii walitoa fatwa zinazoruhusu kutumia mali za dini kwa ajili ya kuanzisha machapisho ya kidini, kielimu na kitamaduni, ili kuongeza kiwango cha uelewa wa jamii kwa ujumla. Uamuzi huu ukawa mwanzo wa kuanzishwa kwa machapisho ya moja kwa moja kutoka katika Hawza."

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha