Shirika la Habari la Hawza - Al-Dhahabi, ambaye anahesabiwa kuwa miongoni mwa nguzo za kielimu kwa Ahl al-Sunna, anasema: “Alikuwa anapewa lakabu ya Jawaad", na "Q'ani" (mwenye kukinai), na "Murtadha" (aliyeridhiwa). Alikuwa miongoni mwa wakubwa wa watu wa Nyumba ya Mtume (s.a.w\.w) na alikuwa mmoja wa waliokuwa wakijulikanwa kwa ukarimu, na kwa sababu hiyo aliitwa "Jawaad”
(Taarikh al-Islam ya Al-Dhahabi, juzuu ya 15, uk. 385)
Hata Ibn Taymiyyah al-Harrani, ambaye anajulikana kwa upinzani wake dhidi ya Shia, kuhusu Imam wa tisa wa Kishia anasema: “Muhammad bin Ali al-Jawaad alikuwa miongoni mwa wakubwa wa Bani Hashim na alikuwa anajulikana kwa ukarimu na utukufu. Hivyo basi, akapewa jina la "Jawaad”
(Minhaj al-Sunna ya Ibn Taymiyyah, juzuu ya 4, uk. 68)
Maneno haya ya wazi na kauli hizi za wanazuoni mbalimbali wa Ahl al-Sunna zinathibitisha kuwa kuitwa kwa Imam wa tisa wa Kishia jina la "Jawaad" si madai ya Shia pekee, bali umaarufu wake katika ukarimu unaonyesha uhalisia kuhusiana naye ambao hauwezi kupingika.
Mfano mwingine wa mapokezi haya ambayo yamenukuliwa katika vyanzo vya Kishia tunaashiria hapa: Tabari al-Shi‘i katika kitabu chake "Dala’il al-Imamah" amenukuu kutoka kwa Ibrahim bin Said kwamba amesema: “Nilimwona Muhammad bin Ali (a.s) akiweka mkono wake juu ya majani ya mzeituni, kisha yale majani yakageuka kuwa fedha mkononi mwake. Nilichukua kiasi kikubwa kutoka kwake na nikayatumia sokoni, lakini hayakupoteza thamani.”
(Dala’il al-Imamah, uk. 398, ya Muhammad bin Jarir bin Rustam al-Tabari al-Amuli al-Saghir)
Maoni yako