Alhamisi 18 Septemba 2025 - 18:13
Hukumu za Kisheria | Kuegemea gari la mtu mwingine pasi na idhini

Hawza/ Mtukufu Ayatullah Khamenei amejibu istiftaa kuhusiana na hukumu ya kisheria ya kuegemea gari la mtu mwingine pasi na idhini.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, katika dunia ya leo, kwa sababu ya msongamano wa watu na maisha ya mijini, mara nyingine hutokea watu, bila kuwa na nia mbaya, kutumia mali za wengine kama vile kuegemea ukuta wa nyumba au gari la mtu mwengine, tatizo hili linahitaji kubainishiwa hukumu ya kisheria ili iwe wazi iwapo tendo hilo linajuzu au la, katika hali ambayo haisababishi madhara yoyote kwenye mali.
Mtukufu Ayatullah Khamenei amejibu istiftaa kuhusiana na mada hii, na jibu linawasilishwa kwenu kama ifuatavyo:

Swali:
Je, kuegemea gari au ukuta wa nyumba ya mtu mwingine bila kupata idhini ya mmiliki (ikiwa hakutakuwa na hasara yoyote), kunajuzu?

Jawabu:
Kunajuzu, isipokuwa katika hali ambayo mtu anajua wazi kuwa mmiliki haridhii kitendo kile.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha