Alhamisi 18 Septemba 2025 - 22:39
Silaha za Muqawama ni Sehemu ya Imani, Azma na Maisha Yetu

Hawza/ Hasan Izzuddin, alisrma kuwa: Kila uamuzi unaopingana na makubaliano na mshikamano wa kitaifa na dhidi ya sehemu yoyote ya Lebanon, unachukuliwa kama dosari ya kikatiba na kitaifa na haukubaliki.

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, Hasan Izzuddin, mjumbe wa kundi la Muqawama na mbunge wa Lebanon, katika hafla ya kumbukumbu ya Hizbullah huko Deir Qanun al-Nahr, alisema: Kila uamuzi unaopingana na makubaliano na mshikamano wa kitaifa na dhidi ya sehemu yoyote ya Lebanon, unachukuliwa kama dosari ya kikatiba na kitaifa na haukubaliki; kwani unakiuka Mkataba wa Taif uliosainiwa mjini Taif, Saudi Arabia, kwa ushirikiano wa Saudi Arabia, Marekani na Syria, na kuletwa baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka kumi na mitano.

Aliongeza kusema: Licha ya makubaliano yaliyopitishwa katika Mkataba wa Taif, serikali ya Lebanon hivi karibuni ilichukua uamuzi dhidi ya silaha za Muqawama, leo kila mtu anajua kwamba sehemu ya kitaifa ya Washia ndiyo ya kwanza kuipa umuhimu kwani ipo kwenye mstari wa mbele dhidi ya adui huyu, pamoja na sehemu nyingine za Wakristo, Masuni na Wadorozi walioko kando ya mpaka wa kimataifa na Palestina iliyochafuliwa kutoka Naqoura hadi Mashamba ya Shebaa.

Izzuddin alisema: Licha ya haya, walikuja kujadili mpango wa taratibu wa kile walichokiita "kuondoa silaha", wakati sisi tuliwashauri kutoka mwanzo kwamba uamuzi huo uliochukuliwa ni kinyume na katiba na unapingana na Mkataba wa Taif, ikimaanisha kwamba uamuzi huu ni kinyume na katiba na hauko kwa moyo wa taifa; kwani ulitokea kutokana na shinikizo la Marekani na Wazayuni, na kuilazimisha serikali kutoa majibu.

Mjumbe wa kundi la Muqawama alisema: Uko wapi uongozi huo wa serikali ambao wafuasi wa uongozi wanajivunia, wale ambao wameweka matumaini yao kwa Marekani, Magharibi, baadhi ya nchi za Kiarabu na adui wa Wazayuni ili kuondoa silaha za Muqawama na kuziangamiza? Marekani kupitia Rais wake Donald Trump, inaitishia Lebanon na serikali yake kuwa waelewe kwamba muda unakaribia kuisha na kama hawatachukua uamuzi wa kuondoa silaha, ina maana kwamba bajeti ya Marekani na nchi za Kiarabu itasitishwa, kwa maneno mengine, anasema kwamba Israel itakuwa huru kabisa kufanya kila jambo kama inavyotaka. Je, hili si tishio la moja kwa moja na kuingilia wazi na kwa ukali masuala ya ndani ya Lebanon?

Aliongeza kusena: Tishio la Wazayuni haliathiri Lebanon tu, bali pia linaathiri kanda yote, na hadi adui huyu atakapokuwa hapa, hawataona utulivu, usalama au amani.

Izzddin alisisitiza: Silaha za Muqawama haziwezi kutenganishwa na sisi, kwani zimekuwa sehemu ya imani yetu, azma na maisha yetu, na zinatupa uwezo na nguvu ya kujilinda dhidi ya adui huyu, kulinda nafsi yetu, taifa, ardhi, heshima na utu wetu.

Mbunge wa Lebanon aliendelea kusema: Pale ambapo silaha zitaondolewa, basi adui ataanza kuiteka Lebanon, katika mfumo wa mpango uliozungumziwa na Netanyahu, ramani ya Israel Kubwa itapandishwa mbele ya dunia yote na kwenye televisheni, kama sehemu ya sera ya kujipanua kijiografia na kudhibiti eneo, hatutaruhusu mtu yeyote kudhoofisha Muqawama; kwani Muqawama ni sababu ya msingi ya nguvu ya Lebanon.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha