Kwa mujibu wa ripoti ya mwandishi wa Shirika la Habari la Hawza kutoka Tehran, Salah Fahsi, mwakilishi wa Harakati ya Amal ya Lebanon nchini Iran, katika kikao cha tatu cha kitaalamu kilichokuwa na mada: “Nafasi ya vyombo vya habari vinavyounga mkono muqawama katika kuwasilisha ukandamizwaji na uthabiti wa watu wa Ghaza” kilichofanyika katika Shirika la Habari la Quds, alikumbusha historia ya muqawama nchini Lebanon, akabainisha nafasi ya Imam Musa al-Sadr katika kubadilisha hali ya Waislamu wa Kishia na kuanzisha Harakati ya Al-Mahrumin, na akazungumzia athari ya njia hiyo katika kuinua hadhi ya kijamii, kiutamaduni na kijeshi ya jamii ya Lebanon.
Mizizi ya Muqawama ndani ya Ashura
Fahs alisisitiza kuwa: “Kiini cha shughuli za muqawama kinarejea kwenye mapambano ya Ashura ya Imam Husayn (a.s.); mapambano yaliyokuwa chimbuko la harakati za uhuru kote katika historia.”
Akaongeza kuwa: “Imam Musa al-Sadr nchini Lebanon, kwa kuongozwa na shule hiyo hiyo, aliweka misingi ya mihimili mitatu ya muqawama: kijeshi, kijamii na kielimu, kupitia hapo aliweza kuwatoa Waislamu wa Kishia Lebanon kutoka pembezoni na kuwapeleka katikati ya mijadala ya kisiasa na kijamii ya taifa.”
Imam Musa Sadri na mabadiliko ya kusini Lebanoni
Mwakilishi wa Harakati ya Amal akifafanua hatua za Imam Musa al-Sadr alisema: “Hapo zamani, Waislamu wa Kishia wa Lebanon hawakuwa na utambulisho wa kitaifa na waliteseka kwa maradhi ya umasikini na kunyimwa haki, Imam Musa al-Sadr kwa kuanzisha shule, hospitali na taasisi za kijamii, alifungua njia mpya, na kwa kuunda Harakati ya Al-Mahrumin, aliweka msingi wa muqawama wa kimfumo.”
Akaendelea kukumbusha: “Imam Musa al-Sadr hata aliwakusanyia misaada ya kifedha Waislamu wa Kishia wahamiaji walioko Afrika, ili fedha hizo zitumike kwa ajili ya maskini na wahitaji wa Lebanon, sera hiyo iliweza kupanda mbegu za kujitegemea na mshikamano miongoni mwa watu.”
Mafanikio ya Miaka 40 ya Muqawama
Fahs akielezea matunda ya njia hiyo alisema: “Leo hii kusini mwa Lebanon kuna zaidi ya shule 450, mtandao wa barabara, umeme na hospitali, maeneo ambayo zamani yalikuwa maskini kabisa sasa yamekuwa miongoni mwa yaliyoendelea zaidi kwa baraka za muqawama.”
Akaongeza kuwa: “Kama zamani hakukuwa na daktari au mhandisi hata mmoja katika familia, sasa katika kila familia kuna angalau daktari au mhandisi, mabadiliko haya yanaonyesha mageuzi makubwa ya kusini mwa Lebanon kutokana na juhudi za Imam Musa al-Sadr na kuendelezwa kwa njia yake.”
Silaha za Muqawama ni Urithi w damu za Mashahidi
Fahs katika sehemu nyingine ya hotuba yake akipinga juhudi za kunyang'anywa silaha Hizbullah alisema wazi: “Tumetoa mashahidi maelfu, na silaha za muqawama ni urithi wa damu yao, silaha hizi hazitatolewa kirahisi.”
Akiuliza swali: “Ikiwa Lebanon haina silaha, ni nani atakayehakikisha kwamba Israel au makundi ya kigaidi ya kitakfiri hayatashambulia nchi hii?”—alisema kwa msisitizo: “Nguvu ya Hizbullah leo inachota nguvu kutoka kwa uungaji mkono wa wananchi, na uwezo huu haupo chini ya harakati nyingine nchini Lebanon; bali katika nyanja nyingi umevuka mipaka yao.”
Salah Fahs alisema: “Marekani na baadhi ya nchi za Kiarabu bado wanafuatilia mpango wa kunyang'anywa silaha Hizbullah, lakini shambulizi la utawala wa Kizayuni dhidi ya Qatar liliwafanya wafuasi wengi wa mradi huu kujiwazia upya, leo hii, kuliko wakati wowote, imebainika kwamba Lebanon bila muqawama mbele ya vitisho vya nje, haitakuwa salama.”
Mwakilishi wa Harakati ya Amal nchini Iran akihitimisha hotuba yake alikumbusha: “Muqawama ni mkakati hai na wenye uhai ambao si Lebanon pekee, bali kanda nzima umewekewa kinga dhidi ya miradi ya Kizayuni.”
Akasema kwa kusisitiza: “Kama Imam Musa al-Sadr alivyoweza kuibadilisha kusini mwa Lebanon kutoka kuwa eneo lililodhulumiwa hadi kuwa eneo lililoendelea na lenye nguvu ya muqawama, vivyo hivyo kuendelezwa kwa njia hii leo kunaweza kuhakikisha heshima na usalama wa mataifa mbele ya uvamizi na njama za madola makubwa.”
Maoni yako