Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza kutoka Tehran, Sheikh Khamis Abbas Mtopa kutoka Tanzania, katika hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa Thelathini na Tisa wa Umoja wa Kiislamu, akigusia umuhimu wa rehema katika mafundisho ya Kiislamu, alisema: Neno “rehema” limetajwa mara nyingi katika Qur’ani, na sisi ni umma wa rehema na umma wa umoja.
Yeye aliongeza kusema: Mtume wa Uislamu (saww) ni Mtume wa rehema na huruma, si kwa wanadamu pekee, bali kwa viumbe vyote.
Sheikh Mtopa aliendelea kugusia masuala ya kisasa na akasema: Tukitazama matukio ya hivi karibuni, je, bado tunaona rehema ndani ya umma? Inatosha kutazama matendo yanayofanywa na utawala wa Kizayuni huko Ghaza.
Yeye alisisitiza: Kama umma wa Kiislamu, tumelazimika kwa umoja na mshikamano kuusaidia Uislamu na kuwasaidia ndugu zetu wa Kipalestina ili ushindi na uadilifu upatikane.
Maoni yako