Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, likinukuu kutoka "Turkpress," kituo hiki kinachojulikana kama "CENTERCIF", kimeanzishwa rasmi chini ya usimamizi wa Mehmet Nuri Ersoy, Waziri wa Utamaduni na Utalii wa Uturuki, katika hafla rasmi iliyofanyika katika Jumba la Makumbusho la Utamaduni wa Anatolia, huku viongozi kadhaa wa ngazi za juu wakiwa wamehudhuria.
Katika hotuba yake, Waziri Ersoy, akichambua vipengele vya kihistoria vya Islamuophobia, amelitaja jambo hili kuwa ni mwendelezo wa sera za kibaguzi na mateso yaliyopangwa katika historia ya mwanadamu, na akaeleza kuwa: "Fikra ya Magharibi inayotegemea ubora wa kimbari (racial superiority) imegeuzwa leo kuwa ni chombo cha kisiasa na kiuchumi kinachotumika kuchochea chuki dhidi ya Waislamu."
Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na viongozi husika, dira ya kimkakati ya kituo hiki itajikita katika nyanja nne muhimu: ufuatiliaji na uthibitishaji wa visa vya chuki dhidi ya Uislamu, utoaji wa msaada wa kisheria na kisaikolojia kwa waathirika, kufanya utafiti wa kielimu, na kuimarisha ushirikiano wa kimataifa. Kadhalika, imepangwa kwamba kituo hiki, kupitia vitengo vyake maalumu, kitashughulikia kufuatilia na kuhifadhi kumbukumbu za visa vya ubaguzi na uchochezi wa chuki dhidi ya Waislamu ulimwenguni kote.
Maoni yako