Jumanne 27 Mei 2025 - 14:17
Ulazima wa Kuchukua Hatua zenye Athari kwa ajili ya Kukomesha Jinai huko Ghaza

Hawza:/ Bw. "Shahbaz Sharif", Waziri Mkuu wa Pakistan, pamoja na ujumbe wake, jioni ya Jumatatu, wamekutana na Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Udhma Khamenei, Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, jioni ya leo katika kikao na Bw. "Shahbaz Sharif", Waziri Mkuu wa Pakistan na ujumbe wake, akibainisha nafasi maalumu ya Pakistan katika jumuiya ya Ulimwengu wa Kiislamu, amesisitiza juu ya haja ya kuwepo kwa harakati za pamoja na zenye athari kati ya Iran na Pakistan ili kukomesha jinai zinazofanywa na utawala wa Kizayuni huko Ghaza.

Kiongozi wa Mapinduzi mwanzoni mwa kikao hiki, akiwa alieleza furaha yake kwa kumalizika vita kati ya Pakistan na India na kueleza matumaini yake ya kupatikana suluhu ya tofauti za nchi hizo mbili, ameeleza pia msimamo mzuri na wa nguvu wa Pakistan katika kadhia ya Palestina katika kipindi cha miaka iliyopita, na kusema: "Katika hali ambayo katika miaka ya hivi karibuni mara kwa mara vimekuwepo vishawishi vya kuanzisha uhusiano kati ya nchi za Kiislamu na utawala wa Kizayuni, Pakistan kamwe haijawahi kuingizwa katika mitego hiyo."

Ayatullah Khamenei, kwa kuashiria uwezo mkubwa wa Umma wa Kiislamu kwa ajili ya kupata nguvu zaidi katika dunia ya leo, ameongeza kusema: "Katika hali ambayo wanaotaka vita duniani wana motisha nyingi ya kuanzisha mifarakano na vita, jambo pekee linaloweza kuhakikisha usalama wa Umma wa Kiislamu ni mshikamano kati ya nchi za Kiislamu na kukuza uhusiano kati ya nchi hizo."

Vilevile, ameielezea kadhia ya Palestina kuwa ndiyo kadhia ya kwanza katika Ulimwengu wa Kiislamu, na kwa kuashiria hali mbaya sana inayo endelea Ghaza, amesisitiza: "Hali ya Ghaza imefikia hatua ambayo watu wa kawaida huko Ulaya na Marekani wanapanga maandamano na kuzikosoa serikali zao, lakini katika mazingira haya haya, kwa masikitiko, baadhi ya serikali za Kiislamu zinasimama upande wa utawala wa Kizayuni."

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, huku akisisitiza kwamba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Pakistan zinaweza, kwa kushirikiana, kuwa na athari katika dunia ya Kiislamu na kuiondoa kadhia ya Palestina katika mkondo huu mbaya, amesema:
"Sisi tuna matumaini mazuri kuhusu mustakabali wa dunia ya Kiislamu, na matukio mengi yanaunga mkono matumaini haya."

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha