Jumatano 28 Mei 2025 - 19:04
Je, pamoja na kuwepo akili, bado tunauhitaji wa dini?

Hawza/ Akili ya mwanadamu pekee haiwezi kutambua viwango vya mema na mabaya kwa kina, na pia haina uwezo wa kuelewa lengo la maisha ya mwanadamu; kwa hivyo, kwa ajili ya mwongozo, tunahitaji dini. Dini inatoa maelezo ya kina ambayo akili haiwezi kuyaelewa.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawzaakili ya mwanadamu katika kutambua kheri na shari na katika kubainisha lengo la maisha, haina uwezo wa kutoa maelezo ya kina, na kwa hiyo inahitaji mwongozo wa dini.

Swali:

Je, akili ya mwanadamu pekee inaweza kutambua mema na mabaya, sahihi na batili? Je, pamoja na kuwa na akili, bado tunahitajia dini?

Jawabu:

Akili hutambua dhana za jumla, na mara nyingi haina uwezo wa kuelewa kwa kina maelezo na mifano ya mambo mbalimbali.

Akili ina uwezo wa kuelewa mema na mabaya ya baadhi ya mambo, si yote, na hata katika mambo hayo machache, mara nyingi haina uwezo wa kufahamu mifano yake kwa undani. Kwa mfano, akili inaweza kuelewa kwa jumla uzuri wa uadilifu na ubaya wa dhuluma, lakini haiwezi kutambua mifano yake, na inapaswa kuuliza dini ili kuelewa.

Akili, pamoja na kwamba inaweza kuthibitisha kuwepo kwa Mwenyezi Mungu, umuhimu wa Siku ya Mwisho na ulazima wa Ujumbe wa Mitume, lakini haina ufahamu wa kina wa maelezo hayo yote.

Akili, kwa sababu haiwezi kubainisha kwa ukamilifu na kwa usahihi manufaa na madhara ya kidunia na ya Akhera, ya kimwili na ya kiroho, ya mtu binafsi na ya kijamii, inanyamaza katika kueleza kwa kina na kubainisha mifano mingi ya mambo.
Kama dini isingetufundisha hukumu nyingi za kifiqhi, kimaadili na za kiitikadi, tusingeyajua kabisa, hasa yale yanayohusu Akhera.

Akili inathibitisha kuwa ulimwengu huu una Muumba ambaye ni Mjuzi na Mwenye Hekima, na kwa hivyo, ulimwengu na mwanadamu havikuumbwa bila lengo au kwa ajili ya ubatili. Hivyo basi, mwanadamu, kama sehemu ya ulimwengu mzima, anaelekea kwenye lengo fulani na ana mwisho maalumu. Hata hivyo, akili haijui lengo la mwanadamu ni nini na mwisho wake ni upi. Kwa hiyo, akili inasema: “Nahitaji dini ili nijue mwanadamu ana lengo gani na anakwenda wapi.”

Dk. Dawud Isfandiyari
Shahada ya Uzamivu katika Itikadi (Kalam) - Taasisi ya Elimu na Utafiti ya Imam Khomeini (r.a.)

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha