Jumatano 28 Mei 2025 - 23:41
Hawza ya Imaam Swadiq (as) yapokea ugeni kutoka katika maktaba ya Sayyed Hakim (ra) Najaf Ashraf nchini Iraqi

Hawza/ Madrasa na hawza ya Imaam Swadiq (as) leo hii imepokea ugeni mzito kutoka katika Maktaba ya Sayyid Hakim (ra), na ugeni huo umekaribishwa vizuri katika hawza hiyo.

Shirika la Habari la Hawza - Hawza ya Imam Swadiq (as) iliyopo jijini Daresalam nchini Tanzania chini ya usimamizi wa samahat sheikh Hemedi Jalala, leo hii tare 28/5/2025 imepokea ugeni ambao ulikuwa ukiongozwa na Hujatul-islam walmuslimina Sheikh Thamir, ugeni huo uliweza kufika katika hauza hiyo na kuonana na wanafunzi pamoja na viongozi wa hauza hiyo.

Moja ya nukta muhimu ambayo inaweza ikawa ni yenye kukumbukwa na wanafunzi kutokana na ujio wa ugeni huo, ni nasaha nzuri ambazo waliweza kuzipata kutoka kwa wanazuoni hao, wanafunzi walihusiwa mambo mbali mbali na maulama hao, mambo ambayo kiuhalisia msomi yeyote yule wa dini kama atashikamana nayo yatamsaidia kukamilisha malengo yake, kwani njia ya kushikamana na elimu ya dini inahitajia subira, uvumilivu na unyenyekevu wa hali ya juu.

Akianza na aya ya Mwenyezimungu mmoja wa geni hao alisema:

«فَلَوۡلَا نَفَرَ مِن كُلِّ فِرۡقَةࣲ مِّنۡهُمۡ طَآئِفَةࣱ لِّيَتَفَقَّهُواْ فِي ٱلدِّينِ وَلِيُنذِرُواْ قَوۡمَهُمۡ إِذَا رَجَعُوٓاْ إِلَيۡهِمۡ لَعَلَّهُمۡ يَحۡذَرُونَ.»

Lakini kwanini hawatoki katika kila kundi miongoni mwao, wakajifunze vyema dini, na kisha waje kuwaonya wenzao watakapo warejea, ili wapate kujihadhari.(Surat tawbah, aya 122)

Alisema kuwa: Moja ya wadhifa muhimu kwa kila mwanafunzi ni kufahamu kusudio na lengo lake lililompelekea yeye kusoma, kwani wapo wengi ambao wanajaribu kuingia katika Jahazi hili la elimu lakini wanaishia njiani na kushindwa kukamilisha malengo yao. Kila mmoja wenu yampasa kufahamu ya kwamba ana umma unao msubiri nyuma yake, na yeye ndie atakae wajibika juu ya umma ule, hivyo basi yampasa kila mmoja wenu aweke bidii zaidi katika masomo kwani atakapo rejea anatazamwa kule kama kiongozi na msomi mahiri wa dini, hivyo jamii itamuelekea yeye na maswali mbali mbali huku ikihitaji majibu ya kutosheleza kutoka kwake.

Hawza ya Imaam Swadiq (as) yapokea ugeni kutoka katika maktaba ya Sayyed Hakim (ra) Najaf Ashraf nchini Iraqi

Mwisho kabisa, ugeni huo ulifanya kikao maalum na viongozi wa juu wa hawza hiyo, ambapo katika kikao hicho waliweza kufahamishwa taratibu zote za kiidara zinazo husiana na hawza hiyo.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha