Jumatatu 15 Juni 2026 - 21:08
Chaguo la Muqawama Limechaguliwa Kwa Msingi wa Kushikamana na Qur’ani Tukufu

Hawza/ Sheikh Ahmad Al-Qattan amesisitiza wa kusema: “Muqawama nchini Lebanon ni uhai wetu, na adui Muisraeli, licha ya kuendelea na mashambulizi yake, ameshindwa kufikia malengo yake.”

Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, Jumuiya ya “Qawluna wal-'Amal” nchini Lebanon, kwa mnasaba wa kuanza mwaka mpya wa Hijria, iliandaa hafla ya kidini na kielimu iliyohudhuriwa na rais wa jumuiya hiyo, Sheikh Ahmad Al-Qattan, katika eneo la Bar Elias.

Katika hafla hiyo walihudhuria Yanāl Sulh, mbunge na mwanachama wa Kambi ya “Uaminifu kwa Muqawama”, Padre Timotheos Abou Rjeili kwa niaba ya Askofu Antonios Al-Souri, wawakilishi wa vyama vya kitaifa na vya Kiislamu, makundi ya Wapalestina pamoja na idadi ya shakhsia mbalimbali katika eneo hilo.

Sheikh Ahmad Al-Qattan katika hafla hiyo alisisitiza kwamba; chaguo la muqawama limechaguliwa kwa msingi wa kushikamana na Qur’ani Tukufu. Akieleza kwamba mradi wa Kizayuni na Marekani unamlenga mwanadamu na ubinadamu kwa ujumla, na kwamba hautofautishi kati ya Waislamu na Wakristo, alisema: “Kusimama pamoja na yeyote anayepambana dhidi ya hujuma za Israeli ni wajibu wa kisheria na Kiislamu.”

Sheikh Al-Qattan aliendelea kwa kusema kwamba; juhudi zinazofanywa na muqawama wa Lebanon kwa ajili ya kumzuia Shetani, na kiwango kikubwa cha kujitolea ambako mashahidi na mujahidina wamejitolea katika kuilinda nchi yao vinapuuzwa.

Mwanazuoni huyo wa Kisunni wa Lebanon alisisitiza: “Muqawama nchini Lebanon ni uhai wetu, na adui Muisraeli, licha ya kuendelea na mashambulizi yake, ameshindwa kufikia malengo yake.”

Aidha alisema: “Tajriba zimeonyesha kwamba; ni nguvu inayofanya mazungumzo, na ni nguvu inayowezesha kupatikana kwa usitishaji wa vita, tunapaswa kumshukuru kila aliyesimama pamoja na Lebanon na kushiriki katika kusimamisha hujuma pamoja na kuchangia katika kuijenga tena nchi.”

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha