Jumatano 28 Mei 2025 - 19:02
Ansarullah Yemen wamehakikisha kuendeleza njia ya Shahidi Sayyid Hassan Nasrallah

Hawza/ Ansarullah Yemen imetoa salamu za pongezi kwa Katibu Mkuu wa Hizbullah, muqawama wa Kiislamu wa Lebanon, na wananchi wa nchi hiyo, kwa mnasaba wa siku ya mapambano na ukombozi wa kusini mwa Lebanon, na imesisitiza kuiendeleza njia ya shahidi wa Uislamu na ubinadamu, Sayyid Hassan Nasrallah (ra).

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawzaofisi ya kisiasa ya Ansarullah Yemen, kupitia taarifa rasmi iliyotolewa kutokana na mnasaba wa kumbukumbu ya mwaka wa 25 tangia ukombozi wa kusini mwa Lebanon, imesema: Tarehe 25 Mei mwaka 2000 tulishuhudia kushindwa kwa fedheha Wazayuni na kuondolewa kutoka kusini mwa Lebanon. Ushindi wa Muqawama wa Kiislamu tarehe 25 Mei 2000 ulitambulisha mabadiliko muhimu ya kimkakati katika muktadha wa mapambano ya Kiarabu na Kiislamu dhidi ya adui Mzayuni.

Taarifa hiyo imeeleza: Kwa ushindi wa wapiganaji wa Hizbullah, umma wa Kiarabu na Kiislamu ulirudishiwa tena imani yake na ujasiri wake, na imani hiyo juu ya uwezo wake iliongezeka mara dufu. Vilevile, ushindi wa Hizbullah dhidi ya adui mwaka 2006 uliweka mipaka na kanuni mpya katika namna ya kushughulika na utawala wa kizayuni unaoukalia kwa mabavu maeneo ya wengine.

Ansarullah Yemen imesema kuwa: Tunasisitiza tena uaminifu wetu kwa Hizbullah na Muqawama, na tutaendeleza njia ya viongozi mashahidi, hususan shahidi wa Uislamu na ubinadamu, Sayyid Hassan Nasrallah (ra). Pia tunatangaza ushirikiano wetu na Lebanon na Muqawama wa Kiislamu, na tunalaani uvamizi na mashambulizi ya mara kwa mara yanayofanywa na Wazayuni dhidi ya ardhi na mamlaka ya Lebanon.

Ansarullah Yemen imetoa wito kwa vyama vya Lebanon kuchukua mafunzo kutoka katika historia, kwani mafunzo haya yanaonesha wazi kuwa nguvu ya Lebanon imo katika muqawama na katika silaha zake, silaha ambazo zimeunda mizania ya kuzuia shambulizi dhidi ya adui Mzayuni.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha