Kwa mujibu wa ripoti ya kikundi cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Isaa Al-Sayyid Muhammad Al-Khurassan, mkuu wa Haram Tukufu ya Imam Ali, alitangaza Jumamosi usiku kuwa zaidi ya wageni milioni 6.3 waliingia katika mkoa wa Najaf Ashraf kwa ajili ya ziara ya Haram tukufu ya Amirul Mu’minin Imam Ali bin Abi Talib (AS).
Al-Khurassan alieleza katika taarifa yake kwamba, kwa mujibu wa vielelezo vilivyorekodiwa na kamera zenye teknolojia ya kuhesabu ya kielektroniki kutoka Kituo cha Teknolojia ya Habari cha Haram ya Amirul Mu’minin (AS), jumla ya wageni waliotembelea Haram ya Amirul Mu’minin (AS) katika kumbukumbu ya shahada yake walifikia milioni 6 laki 391 elfu na 390.
Maoni yako