Kwa mujibu wa kundi la tarjuma la Shirika la habari la Hawza, Sayed Sajid Ali Naqvi, kiongozi wa Baraza la Maulama wa kishia Pakistan, katika ujumbe wake kwenye maadhimisho ya siku ya kuzaliwa Imam Hasan al-Mujtaba (A.S.), alisisitiza umuhimu wa umoja na mshikamano kati ya Waislamu.
Kiongozi huyo aliashiria kuhusiana na tabia nzuri ya Imam Hasan (A.S.) na alisema: “Sisi kwa kutumia maadili ya kiungwana na tabia ya amani aliyokuwa nayo Imam Hasan (A.S.), tumejitahidi kueneza hali ya umoja na undugu katika ardhi yetu tukufu ya Pakistan, umoja huu umeilinda nchi dhidi ya migawanyiko na machafuko na pia umeunganisha watu wa Pakistan katika silsila ya undugu na upendo."
Mwanzuoni huyu maarufu wa Pakistan aliendelea kusema: "Kueneza umoja kati ya Waislamu na kuimarisha undugu na mshikamano ni wadhifa wetu wa kidini na Kiislamu. Katika kipindi hiki kigumu ambacho umma wa Kiislamu unakutana na changamoto za ufarakanishi wa kimadhehebu, itikadi kali, ugaidi, na matatizo ya kimaadili, ni muhimu kuiweka mbali migawanyo midogo midogo na kuyatilia mkazo yale yaliyo ya pamoja, pamoja na kuchukua hatua madhubuti ili kukuza umoja wa umma wa Kiislamu."
Maoni yako