Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawzat, Hojjat al-Islam wal-Muslimin Nasir Rafiei, akizungumzia siku njema na tukufu za Mwezi wa Rajab, alisema katika mkutano huu kuwa: Mtukufu Mtume wa Uislamu (amani iwe juu yake) alimwambia Amirul Muuminina Ali bin Abi Talib (a.s) katika riwaya yenye vipengele arubaini: Mwenye kufanya hima juu ya haya 40 na akayaweka katika uhai wake; atakwenda Peponi naye atakuwa mbora wa watu baada ya Manabii na watu wema (wasema kweli), na Mwenyezi Mungu atamfufua pamoja na Mashahidi, Manabii na watu wema Siku ya Kiyama.
Aliendelea kueleza baadhi ya yaliyomo katika riwaya hii na kukumbushia kuwa: Mtume (s.a.w.w) alimwambia Imam Ali (amani iwe juu yake) kuwa kamwe asiipende Dunia kuliko Akhera kwa sababu Dunia ni ya kutoweka na Akhera inabakia.
Hadhrat Muhammad (s.a.w.w) anasema kwamba usiwe bakhili katika kuwatumikia watu, na jambo lingine ni kwamba sura yetu ya ndani na ya nje inapaswa kuwa sawa.
Hojjat al-Islam wal-Muslimin Rafiei aliendelea kubainisha: "Kujizoeza wewe mwenyewe, familia yako, jamaa na marafiki kwa kadiri ya uwezo wako na kufanya kile ambacho una uhakika nacho ni (nasaha) mapendekezo mengine mawili ya Mtume wa Mwenyezi Mungu yaliyopo katika riwaya hii."
Maoni yako