Kwa mujibu wa taarifa kotoka katika idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, kutokana na uvamizi wa mara kwa mara unaofanywa na Marekani pamoja na utawala wa Kizayuni dhidi ya taifa la Palestina, {kongamano la kuwaunga mkono Palestina} limefanyika katika jiji la Karachi, Pakistan huku likihudhuriwa na viongozi wa kisiasa, kidini, wasomi wa vyuo vikuu na watu wengine tofauti.
Katika kongamano hilo, ilibainishwa waziwazi kwamba, wale wote wanaopinga dhana ya ukombozi kwa Palestina ndani ya Pakistan ni maadui wa Pakistan. Katika kuliweka sawa hili, maneno ya kihistoria ya Muhammad Ali Jinnah yalinukuliwa kama rejea, ambapo alilitaja taifa la Israel kuwa ni taifa lisilo na uhalali, na kusisitiza kuwa Pakistan kamwe haiwezi kulitalitambua taifa hilo.
Maoni yako