Jumatatu 7 Aprili 2025 - 09:52
Mjadala uliojiri kati ya Marehemu Ayatollah al-Udhma Fazel Lankarani na Imamu wa kipindi hicho wa Msikiti wa Haram

Safari moja nikiwa Makka, nilikutana na mzee mmoja ambaye alisema kuwa alikuwa Imamu wa msikiti mtakatifu wa Haram kwa kipindi cha miaka kumi. Umri wake haukuruhusu tena kuendelea kuwa imamu. Miongoni mwa mambo niliyomuuliza ni hili: “Kwa nini katika maktaba zenu hakuna vitabu vya kishia, na ilhali katika maktaba zetu kuna vitabu vya madhehebu yenu?”

Shirika la Habari la Hawza - Mazungumzo haya ya marehemu Ayatollah Sheikh Muhammad Fazel Lankarani yamechapishwa katika kuelekea kumbukizi ya siku ya kubomolewa makaburi ya Maimamu wa Baqii (a.s).

Safari moja nikiwa Makka, nilikutana na mzee mmoja ambaye alisema kuwa alikuwa Imamu wa msikiti mtakatifu wa Haram kwa kipindi cha miaka kumi. Umri wake haukuruhusu tena kuendelea kuwa imamu. Miongoni mwa mambo niliyomuuliza ni hili: “Kwa nini katika maktaba zenu hakuna vitabu vya kishia, ilhali katika maktaba zetu kuna vitabu vya madhehebu yenu?, Sisi tuna tafsiri zenu za Qur’ani, vitabu vya historia pamoja na vitabu vyenu vya hadithi. Mimi binafsi ninacho kitabu cha "Kanzu al-‘Ummāl" ambacho huenda kikawa ni mojawapo ya vitabu vikubwa kabisa vya riwaya za Ahlus-Sunna.
Pia ninavyo vitabu vya tafsiri kama vile "Tafsīr al-Zamakhshari" na "Tafsīr Fakhr al-Rāzī", na katika fiqhi ninacho kitabu cha "al-Muḥallā cha Ibn Ḥazm", na vitabu vinginevyo vingi.

Nikamuuliza tena, “Kwanini maktaba zenu hazina hata kitabu kimoja cha Kishia, lakini sisi tunaweka vyenu?” Hakunijibu chochote. Nikamwambia, “Je, utaniruhusu mimi nikujibu mwenyewe?” Akasema, “Naam, endelea.” Nikasema, “Jawabu ni kwamba: Sisi hatuogopi kuwepo vitabu vyenu katika maktaba zetu kwa sababu sisi tupo katika haki ya dhahiri, lakini ninyi mnaogopa kuwepo vitabu vyetu kwenye maktaba zenu kwa sababu mko katika batili, Mnahofia kwamba anaweza akaja mtu kufanya tahakiki kuhusu ushia, na hatimae akaelewa ukweli kuhusu madhehebu ya kishia, kwa sababu hiyo hamtaki kuruhusu vitabu vyetu viwepo katika maktaba zenu.”

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha