Jumatatu 7 Aprili 2025 - 09:45
Tukio la kubomolewa makaburi ya maimamu wa Baqii (a.s) halina mbadala

Marehemu Ayatollah Safi Golpayegani katika chapisho alilo liandika kuhusiana na mnasaba wa kumbukizi ya kubomolewa kwa makaburi ya Maimamu wa Baqii (a.s), alieleza wazi kuwa: Lengo ovu la maadui katika udhalilishaji huu mkubwa lilikuwa ni kuharibu nguzo za historia ya uislamu pamoja na nyaraka na athari zake za kihistoria.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, chapisho hili la marehemu Ayatollah Safi Golpayegani lilichapishwa kwa mnasaba wa tarehe nane Shawwal, siku ambayo inasadifu kumbukizi ya kubomolewa makaburi ya Maimamu wa Baqii (a.s).

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu

Mwenyezi Mungu amesema: “Katika nyumba ambazo Mwenyezi Mungu ameruhusu zitukuzwe na litajwe humo jina Lake…”

Katika tafsiri ya aya hii tukufu, kama ilivyoelezwa katika vitabu mashuhuri vya tafsiri kwa mfano "Ad-Durr al-Manthur" ya Suyuti, imepokelewa kuwa Mtume (s.a.w) aliulizwa: Je! Nyumba hizi tukufu zinazotajwa katika aya hii ni nyumba za kina nani?

Akasema: “Ni nyumba za Manabii.”

Kisha Abu Bakr akauliza huku akielekeza mkono wake kwenye nyumba ya Ali na Fatima (a.s): “Je, hii ni miongoni mwa nyumba hizo?”

Mtume (s.a.w) akajibu: “Ndiyo, na ni miongoni mwa nyumba bora zaidi.”

Tarehe nane Shawwal siku ya Kimataifa ya Baqii

Baqii, kwa zaidi ya karne kumi na nne sasa, imekuwa ni sehemu ya kuzuru waislamu, na ni markaz ya kuamsha fikra na kukumbushia historia ya viongozi wakubwa waliopita katika uislamu.

Makaburi haya, baada ya kaburi takatifu la Mtume (s.a.w), ni miongoni mwa vyanzo muhimu vya historia ya uislamu vinavyothibitisha uwepo wa shakhsia mbalimbali za kiislamu, ambapo inakadiriwa kuwa takriban Maswahaba elfu kumi wa Mtume Mtukufu (s.a.w) wamezikwa katika makaburi haya.

Waislamu wengi wanahuzunika juu ya kudhalilishwa historia ya uislamu

Hata hivyo, licha ya utukufu mkubwa wa eneo hili tukufu, hali yake ya sasa ni ya kufedhehesha sana, na udhalilishwaji uliofanywa kwa watu wazito walio zikwa hapa ni wa kusikitisha mno na kuhuzunisha.

Hakuna sehemu yoyote duniani ambapo watu huyakosea adabu na heshima makaburi ya watu wao mashuhuri kama ilivyofanyika hapa. Kila mahali ambapo kuna  makaburi, watu wanayaheshimu makaburi hayo.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha