Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, taarifa ya Kituo cha Usimamizi wa Hawza kutokana na mnasaba wa tarehe ya kumbukumbu ya kuharibiwa makaburi matukufu ya Maimamu wa Baqii (a.s), maelezo ni kama ifuatavyo:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu
Katika siku ya kumbukizi ya tukio kubwa na la kusikitisha la kubomolewa kwa makaburi matukufu ya Maimamu wanne (a.s) katika makaburi ya Baqii, tena kwa mara nyingine mioyo ya waumini na wapenda haki duniani kote hususan wapenzi wa Ahlul-Bayt (a.s) imejeruhiwa.
Jinai hii kubwa ilitokea tarehe 8 Shawwal mwaka 1344 Hijria, na haikuwa tu ni dharau kwa Ahlul-Bayt (a.s) na historia ya uislamu, bali ilikuwa ni alama na fikra ya kigaidi, fikra isiyo ya kiislamu ambayo matokeo yake yamekuwa ni vurugu, migawanyiko, na kupotosha sura halisi ya uislamu.
Kituo cha Usimamizi wa Hawza, kinaendelea kuiheshimu nafasi tukufu ya Ahlul-Bayt wa Mtume (a.s), na kulaani vikali tukio hili la kihistoria. Aidha, kinasisitiza kuwa, ujenzi wa makaburi haya matukufu ni hitaji la kimataifa kutoka kwa umma wa kiislamu, na ni madai ya wazi kutoka kwa maraaji na wanazuoni wakubwa wa Hawza.
Kadhalika, katika siku hizi dhulma zinazo fanyiwa waislamu katika nchi za Yemen, Gaza, Lebanon, Bahrain, Afghanistan, Pakistan na maeneo mengine ya kiislamu, chini ya mashambulizi ya kikatili, na huku jumuiya za kimataifa zikinyamazia dhulma hizi, ni ushahidi tosha wa kuendelezwa kwa fikra ile ile potofu na ya kigaidi ambayo jana iliharibu makaburi ya Baqii, na leo hii inaendelea kumwaga damu ya watoto, wanawake na raia wasio na hatia.
Jinai ya hivi karibuni iliyo fanywa na utawala wa Kizayuni huko Gaza ni mauaji ya halaiki na ya kinyama, yanayotekelezwa kwa msaada wa madhalimu na watawala vibaraka, hali ambayo inahitajia umma wa kiislamu kuwa na umoja, uelewa, na kuchukua hatua za haraka.
Markaz ya usimamizi wa Hawza, ikiwa ni yenye kushikilia mafundisho yenye nuru ya Qur’an na Ahlul-Bayt, inawaomba wanazuoni na wasomi katika ulimwengu wa kiislamu wavunje ukimya wao kuhusu jinai hii, na wahakikishe umma wa kiislamu unasimama pamoja, kuwatetea wanyonge, na kushiriki katika ujenzi wa maeneo matakatifu.
“Na wale wanao dhulumu watakuja jua mgeuko gani watakao geuka".
Makao makuu ya Hawza
Maoni yako