Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul Islam wal-Muslimin Muhammadi Iraqi, mwanzoni wa somo lake la kwanza la kiwango cha juu katika mwaka mpya wa Shamsi, alisema: “Kwa masikitiko makubwa, tena katika masiku haya ya mwezi mtukufu wa Ramadhani na Sikukuu ya Idd Fitr, maisha ya ndugu zetu wanyonge wa Palestina yalichafuliwa kwa mashambulizi mapya ya ardhini na kuwafanya wawe wakimbizi tena. Watu wa Gaza na Lebanon hawakupata hata na fursa ya kufuturu kwa utulivu usiku. Leo hii pia katika kalenda ya kimataifa, siku hii imetajwa kuwa ‘Siku ya Mtoto wa Kipalestina’. Haya ni miongoni mwa maajabu ya zama hizi, na ni tukio kubwa linalopaswa kusajiliwa katika historia kwamba katika karne ya 21, ndani ya ustaarabu wa Magharibi, huku kukiwa na madai juu ya haki za binadamu, jinai za kuwaua watoto zimejirudia kama ilivyokuwa katika kipindi cha Firauni.”
Raisi huyo wa ofisi ya Kiongozi Mkuu katika mji wa Qom alieleza kuwa, katika mashambulizi yaliyo fanywa hivi karibuni, idadi kubwa ya watoto wa Kipalestina wameuawa kishahidi, na wengine wengi wako hatarini kutokana na njaa, ukosefu wa dawa na mashambulizi ya mabomu kwenye hospitali, alisema kwamba: “Ukatili huu dhidi ya watoto unatukumbusha jinai za Firauni katika enzi za Nabii Musa (a.s), ambapo aliagiza watoto wa Bani Israil wauawe. Lakini tofauti kubwa ni kwamba wakati ule ulikuwa ni wakati wa ujinga, unyama na ukatili wa binadamu, lakini sasa hivi tuko katika zama zinazodai kuenzi haki za binadamu na demokrasia, na bado jinai hizi zinatendeka na hakuna anayezipazia sauti.”
Aliendelea kueleza tofauti kali kati ya mauaji ya Firauni na haya yanayofanywa na utawala wa Kizayuni: “Firauni alikuwa anawaua tu watoto wa kiume, lakini leo hii, utawala wa Kizayuni unashambulia bila kujali jinsia, umri au hali ya mtoto, wake na wanaume wa Palestina wanawavamia. Watoto hawa hawana hatia yoyote, na hakuna ishara kwamba watawahi kuwa tishio kwa utawala huo, jinai hii ni ya kipekee katika historia, na kwa masikitiko, kunyamaza jumuiya za kimataifa na serikali za Magharibi hasa Marekani kumezidi kuchochea jinai hizi.”
Hujjatul Islam wal-Muslimin Muhammadi Iraqi alihitimisha kwa kusema: “Cha kushangaza zaidi ni kunyamaza na kutojali kutoka katika baadhi ya nchi za kiarabu na kiislamu. Si tu kwamba wamenyamaza, bali katika baadhi ya nyanja wanatoa msaada wa wazi au wa kificho kwa utawala wa Kizayuni na kushirikiana nao. Hii ni aibu kubwa na ndiyo fedheha kubwa zaidi katika historia.
Maoni yako