Kwa mujibu wa idara ya tarjuma ya Shirika la Habari la Hawza, kufuatia mikutano ya Umoja wa Mataifa, nje ya jengo la Umoja wa Mataifa, Petro katika hotuba yake alitoa wito wa kuundwa umoja mkubwa wa kimataifa ili kumaliza vita vya Ghaza, katika hotuba yake alisema: “Nguvu ya umoja huu wa kimataifa lazima iwe kubwa kuliko Marekani.”
Aliendelea kusema: “Kwa sababu hiyo leo niko hapa ili kuwaomba wanajeshi wote wa Marekani kwamba wasiwalenge watu kwa silaha zao, wasimfuate Trump bali waisikilize sauti ya ubinadamu na utu, na wafuate dhamiri ya kibinadamu.”
Katika hotuba yake kwenye Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Petro aliikosoa vikali serikali ya Trump na kusisitiza kwamba Rais wa Marekani “ni mshirika katika mauaji ya kimbari” ya watu wa Ghaza.
Baada ya hotuba zake hizi za kishujaa na za kibinadamu, serikali ya Marekani kwa kitendo kilichoitwa cha udhalilishaji, ilimfutia viza yake.
Chanzo: MIDDLE EAST EYE
Maoni yako