Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Akizungumza na vyombo vya habari leo Jumatatu mjini Singida, katibu wa BAKWATA mkoa wa Singida, alhaj omar muna, alisema kuwa uchaguzi huo uliofanyika jana Jumapili ulihusisha nafasi mbalimbali zikiwemo mwenyekiti wa halmashauri ya mkoa, wajumbe wa baraza la masheikh, pamoja na mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa anayewakilisha mkoa wa Singida.
Kwa mujibu wa taarifa yake, mjumbe wa halmashauri kuu BAKWATA taifa anayewakilisha mkoa wa Singida amechaguliwa Abdallah Ramadhani kundya, huku nafasi ya mwenyekiti wa halmashauri ya mkoa ikichukuliwa na Omary Hamisi Mung’nyi.
Aidha, wajumbe waliochaguliwa kuunda baraza la masheikh la mkoa wa Singida ni kama ifuatavyo:
1. Sheikh Salumu Juma Ng’aida
2. Sheikh Ramadhani Suleiman Ibrahim
3. Sheikh Muhamad Juma Ihucha
4. Sheikh Ibrahim Ally Ibrahim
5. Sheikh Hemed Said Mwinshehe
6. Sheikh Abdu Omary Shakitila
7. Sheikh Shaban Omary Wawa
8. Sheikh Seleman Omary Hanje
9. Sheikh Nawawi Salimu Itara
Kwa upande wa halmashauri ya BAKWATA mkoa wa Singida, waliopata nafasi ni:
1. Juma Athuman Ntandu
2. Rajabu Shabani Mussa
3. Mohamed Salum Msaghaa
4. Omary Abbakar Ally
5. Said Abdalla Mwangu
6. Shaibu Swalehe Simba
7. Ibrahimu Abduly Sharifu
8. Athumani Adamu Mzee
9. Juma Ally Mande
10. Juma Hassani Mande
Wajumbe watatu wa halmashauri hiyo walioteuliwa na sheikh wa mkoa ni:
1. Mung’enyi Senge Mung’enyi
2. Hajj Mohamed Mtulia
3. Hassan Mtatuu Dumwala
Akizungumza kwa niaba ya ofisi ya mkoa, alhaj muna aliwapongeza wote waliochaguliwa na kuteuliwa, huku akiwataka kutambua kuwa majukumu yao ni ya wito na ibada, hivyo wafanye kazi kwa moyo wa uadilifu na kujituma kwa ajili ya maslahi ya umma wa kiislamu.
“Tunawaomba viongozi hawa wapya wazingatie kuwa kazi zao ni za kutumikia dini, si za kujinufaisha binafsi. Malipo yao halisi ni kutoka kwa Allah,” alisema alhaj muna.
Katibu huyo pia aliwashukuru viongozi wa BAKWATA taifa kwa usimamizi bora wa uchaguzi huo, akiwataja mwenyekiti wa halmashauri kuu, Sheikh Khamisi Mataka, na Alhaj Swedi Twayyub, pamoja na msimamizi wa uchaguzi Mwalimu Rashid, kwa kuhakikisha mchakato unafanyika kwa amani, haki na uwazi.
“Huu ulikuwa uchaguzi wa mfano, uliosimamiwa kwa uadilifu mkubwa. Tunatarajia mikoa mingine nayo itafuata utaratibu huu katika chaguzi zijazo,” aliongeza alhaj muna.
Kwa kufanyika kwa uchaguzi huu, mkoa wa Singida sasa unakuwa miongoni mwa mikoa iliyokamilisha kikamilifu taratibu za uchaguzi wa viongozi wa BAKWATA mwaka 2025.
Mughanga – Singida
Maoni yako