Jumatano 8 Oktoba 2025 - 11:00
Wanigeria watangaza kuwaunga mkono Watu Wanyonge wa Palestina

Hawza/ Wafuasi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria na wafuasi wa Sheikh Ibrahim Yaqub Zakzaky walishiriki katika maandamano makubwa, wakitangaza msimamo wao wa kuikemea Israeli na kuiunga mkono Palestina.

Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, watu wa Nigeria katika maandamano haya walitangaza kwa uwazi kwamba kamwe hawataitambua Israeli kama nchi halali na walilaani uhalifu wa kinyama unaofanywa na utawala huo haram.

Imesisitizwa kuwa utawala wa Israeli ni zao la fikra za kishetani, na watendaji wakuu wake hawapokei maagizo kutoka kwa yeyote isipokuwa Shetani, na misingi yake imejengwa juu ya dhulma, ukosefu wa haki na damu ya wanyonge.

Wafuasi wa Sheikh Ibrahim Yaqub Zakzaky, kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria, katika maandamano haya walisema:


Sisi tunasimama bega kwa bega na ndugu zetu Wapalestina — wanaume na wanawake — na tunatoa wito kwa watu wote duniani kuwaunga mkono watu wanyonge wa Ghaza.

Chanzo: Tovuti rasmi ya Harakati ya Kiislamu ya Nigeria

Maoni yako

You are replying to: .
captcha