Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Katibu wa BAKWATA Mkoa wa Singida, Alhaj Omar Muna, amesema uchaguzi huo umefanyika kikamilifu, na wenyeviti wapya waliopatikana katika kila wilaya ni:
1. Irambo – Ally Abdallah Katembo
2. Singida Mjini – Hamisi Mohamed Kisuke
3. Manyoni – Juma Shabani Kamili
4. Itigi – Khamisi Mrisho Ikumbu
5. Mkalama – Muadhi Mussa Ntoga
6. Singida Vijijini – Iddy Hamisi Isango
7. Ikungi – Mwl. Selemani Joseph Memba
Aidha, kila wilaya imefanikiwa kupata wajumbe saba wapya wa Baraza la Masheikh na wajumbe 10 wapya wa Halmashauri za BAKWATA wilaya husika.
Alhaj Muna ameongeza kuwa hatua zilizobaki ni ngazi ya mkoa, ambapo fomu kwa waombaji wa nafasi za mkoa tayari zimetolewa kuanzia Jumatatu. Uchaguzi wa mkoa utafanyika tarehe 12 Oktoba 2025.
Katibu huyo pia amebainisha kuwa uchaguzi wa ngazi ya msikiti na kata tayari umefanyika, na hatua ya sasa ni kuendelea na uchaguzi wa ngazi ya mkoa ili kukamilisha mchakato mzima wa uchaguzi wa BAKWATA mkoa wa Singida.
Maoni yako