Kwa mujibu wa kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Siku ya ziara hiyo, msikiti wa Preston uliwaalika wananchi wote kuja kupata maarifa zaidi kuhusiana na dini ya Uislamu pamoja na jamii ya Waislamu wa eneo hilo, vile vile na kuuliza maswali kuhusu masuala yanayowahusu.
Wageni waliokaribishwa walipata mapokezi mazuri, huku mwongozaji wageni akielezea historia ya msikiti huo na nafasi yake katika maisha ya kila siku ya watu — si tu kama mahali pa ibada, bali pia kama kitovu cha kitamaduni na kijamii kinachochangia katika kukuza tabia njema na maendeleo binafsi. Pia alizungumzia umuhimu wa adhana katika msikiti na wajibu wake kwenye jamii ya Kiislamu.
Ndani ya ukumbi mkuu wa msikiti, wageni walipata nafasi ya kutembelea maonesho ya sanaa za Kiislamu na uandishi wa Kiarabu, huku wakipewa maelezo mafupi kuhusu historia ya Uislamu katika karne mbalimbali pamoja na urithi wa kisanaa na kiroho wa Waislamu.
Ismail Timol, mmoja wa waandaaji wa hafla hiyo ya ziara ya wazi, alisema: “Tulifurahia sana kuwa wenyeji wa watu wengi waliotoka katika asili na mitazamo tofauti. Ni ile hamu ya kujua na roho ya upendo inayotuleta pamoja kama jamii.”
Chanzo: Yahoo News
Maoni yako