Jumanne 8 Aprili 2025 - 19:30
Masharti ya Kufidia Hasara katika mkataba wa Mudharaba

Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Ali Khamenei, amejibu swali kuhusu "sharti la kufidia hasara katika mkataba wa mudh'araba".

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Khamenei alijibu swali lililohusu "sharti la kufidia hasara katika makubaliano ya Mudharaba" na jawabu lake ni kama tunavyo kufahamisha.

sharti la kufidia hasara katika makubaliano ya Mudh'araba

Swali:
Je, katika makubaliano ya mudh'araba, mwekezaji anaweza kuweka sharti kwamba, wakala wa biashara (mudharib) atawajibika kufidia hasara zote zinazoweza kutokea katika mtaji kutoka kwenye mali zake binafsi?

Na iwapo faida haitapatikana kutoka katika muamala huo, je, mwekezaji anaweza kudai faida kutoka kwa wakala?

Jawabu:
Kuweka sharti la kufidia hasara kama hilo hakuna tatizo, lakini ikiwa faida haitapatikana, mwekezaji hawezi kumlazimisha wakala kutoa faida.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha