Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatollah Jawadi Amoli katika mazungumzo yake alizungumzia mada ya “Umuhimu wa kukumbuka mauti na nafasi yake katika kuleta uchamungu (taqwa)” na akasema:
“Mara kwa mara mmekuwa mkisikia kwamba baadhi ya watu wanatafuta dhikri, huku wakiuliza: 'Ni dhikri ipi itakayo tukurubisha na Mwenyezi Mungu?' na mfano wa hayo.
Baadhi ya wanazuoni wakubwa na wenye maarifa waliandika risala fupi, wakisema: Tumetembea sehemu nyingi, tumekutana na wanazuoni wengi, tumesoma na kusikia maneno mengi, lakini hatukuona dhikri yoyote yenye athari zaidi baada ya kumkumbuka Mwenyezi Mungu mtukufu kama vile kukumbuka mauti.
Hakuna dhikri yeyote ile baada ya kumdhukuru Mwenyezi Mungu inayo lingana na kukumbuka Mauti. Je! Unatafuta kitu gani hasa! Inatosha kwa mtu kukumbuka mauti, mauti ndiyo yanavunja matamanio ya kidunia, tukitaka kumkaribia Mwenyezi Mungu, ni lazima tukumbuke mauti.
"Tukitaka kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu, ni lazima tukumbuke mauti. Mwanazuoni huyu katika risala yake anasema: Sijaona dhikri yoyote yenye athari kubwa zaidi baada ya dhikri ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kama kudhukuru mauti. Dhikri hiyo humfanya mtu kuwa mchamungu; kwani ikiwa mtu atakumbuka kifo, basi bila shaka hiyo si kazi rahisi kuondoka duniani mikono mitupu huku uso wake ukiwa umejawa na aibu, hilo ni jambo gumu sana, hivyo basi, kwa hali ya kawaida mtu huyo mda wote atakuwa anafikiria kuhusu uchamungu."
Maoni yako