Jumatano 1 Aprili 2026 - 06:00
Tunaiunga mkono Hizbullah katika kuilinda Lebanon

Hawza/ "Mkusanyiko wa Wanazuoni Wakiislamu wa Lebanon" umesema katika taarifa yake kwamba; Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imethibitisha kuwa ni nchi yenye nguvu; kwa namna ambayo mauaji ya kinyama yaliyowalenga viongozi hayakuweza kuiathiri.

Kwa mujibu wa kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, kamati ya idara ya "Mkusanyiko wa Wanazuoni wa Lebanon" imesema katika taarifa yake baada ya mkutano wake wa kawaida kwamba: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imethibitisha kuwa ni nchi yenye nguvu na yenye miundo imara ya kikatiba; kwa namna ambayo mauaji ya kinyama yaliyowalenga viongozi—ikiwa ni pamoja na Imam Sayyid Ali Khamenei—na ya hivi karibuni zaidi ikiwa ni mauaji ya Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa, Ali Larijani, na Kamanda wa Basij, Saardr Gholamreza Soleimani, hayakuweza kuiathiri. Iran imeweza kuingia vitani mara moja bila kuchelewa, na katiba imewawezesha viongozi wa Iran kutoa warithi, ambapo matokeo yake ilikuwa kuchaguliwa kwa Ayatullah Sayyid Mujtaba Khamenei kama Msimamizi wa Walii faqihi wa Umma.

Taarifa hiyo imeongeza: Urushaji wa makombora ulianza hatua kwa hatua katika kiwango na ukubwa wake, na kuonjesha uchungu wa matokeo kwa adui wa Kizayuni; sasa adui amechanganyikiwa na anajaribu kulipa kisasi kwa kutoshindwa kwake kwa kushambulia miundombinu isiyo ya kijeshi, kulipua maeneo ya makazi, hospitali na maghala ya mafuta. Wakati majeshi ya Iran yanayolenga vituo vya kijeshi na kambi za Marekani katika eneo hilo, na wamechukua hatua katika Ghuba ya Hormuz ambazo zimeathiri uchumi wa nchi mbalimbali hasa uchumi wa shetani mkuu, Marekani.

Mkusanyiko wa wanazuoni umeendelea kusema: Donald Trump aliomba msaada kutoka kwa washirika wake wa Ulaya na viongozi tegemezi duniani ili kufungua Mlango wa Hormuz; lakini walimwacha peke yake ili akabiliane na mgogoro mkubwa. Leo yupo kati ya chaguzi mbili: Ima kuondoka katika vita hivi bila chochote, bila kutimiza lengo hata moja au kuendeleza vita, vita ambavyo vitamuingiza katika mgogoro wa ndani ambao dalili zake zimeonekana katika matamko yake yanayokinzana na kujiuzulu kwa mkurugenzi wa idara ya kupambana na ugaidi.

Taarifa hiyo iliashiria kuwa: Nchini Lebanon, Hezbullah inafanya operesheni za kishujaa kukabiliana na juhudi za Wazayuni; juhudi ambazo hadi sasa hazijaweza kufikia maendeleo yoyote yanayoonekana. Adui anasonga mbele hatua moja na anarudi nyuma hatua kadhaa chini ya mashambulizi ya muqawama.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha