Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, matini ya barua ya Ayatollah Nouri Hamedani kwa Papa Leon wa kumi na nne, kiongozi wa Wakatoliki duniani, ambayo imetolewa kupitia balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran huko Vatican, ni kama ifuatavyo:
Bismillahir Rahmanir Rahim
Mheshimiwa Papa Leon wa Kumi na Nne
Kiongozi wa Wakatoliki Duniani
Kwa salamu na heshima
Kama ambavyo mnafahamu, heshima ya mwanadamu inayomaanisha utukufu, ukuu na thamani ya asili ya binadamu, ni miongoni mwa dhana za msingi katika dini za kimungu. Dini zote za Ibrahimu zimeelekeza msisitizo kwa hadhi ya juu ya mwanadamu na kumwona mwanadamu kuwa ni kiumbe chenye thamani ya asili na uwezo wa kiroho, aliyeumbwa kwa namna maalumu na Mwenyezi Mungu, dini zote za kimungu zinathibitisha kanuni ya usawa, uhuru, uwajibikaji na haki za binadamu, na zinakanusha kwa nguvu ubaguzi wa kikabila, kimataifa na kitabaka.
Ni dhahiri kuwa dini za kimungu, licha ya tofauti zao za kiitikadi, zinakubaliana katika kusisitiza heshima ya asili ya mwanadamu, heshima hii si tu msingi wa haki za binadamu, bali pia ni njia ya kuweka uhusiano wa kimaadili na kibinadamu baina ya wafuasi wa dini mbalimbali. Katika dunia ambayo ghasia na ubaguzi vinaongezeka, kurejea kwenye msingi huu wa pamoja kunaweza kuwa njia inayokubalika kwa ajili ya kuishi kwa amani na kuelewana baina ya dini.
Kama mnavyojua, Ghaza ni ardhi iliyozingirwa ambayo leo imekuwa alama ya dhulma dhidi ya mwanadamu mbele ya dhulma na ukosefu wa haki, wakati ambapo dunia inashuhudia vifo vya kila siku vya watoto, wanawake na wanaume wasio na hatia kutokana na njaa, kiu na uhaba wa dawa, utawala wa Kizayuni ukiwa unaendeleza kuizingira Ghaza na kuzuia kuingia kwa chakula na misaada ya kibinadamu, umesababisha janga lisilo na kifani katika historia ya kisasa, tabia hii haikubaliki si kwa mtazamo wa kibinadamu, wala wa kidini, kimaadili au hata sheria za kimataifa.
Uislamu ni dini ya rehema na mapenzi kwa wanadamu, na kuwasababishia mateso watu wasio na hatia—hasa watoto na wanawake—kumekemewa kwa nguvu sana Katika mafundisho ya Kikristo pia, kusaidia wenye njaa na wahitaji ni jukumu la kimungu, na katika Taurati pia kuna msisitizo mkubwa juu ya haki na huruma kwa wengine, kutoka katika mtazamo wa dini za kimungu, kuwanyima watu chakula ni dhulma kubwa inayokwenda kinyume na mapenzi ya Mwenyezi Mungu.
Pia kwa mtazamo wa maadili ya kibinadamu na dhamira zilizo hai, kuwazingira mamia ya maelfu ya watu wasio na hatia, wakiwemo wanawake na watoto, na kuwaletea mashinikizo pamoja na mashambulizi ya kinyama huku wakizuiwa kupata chakula na dawa, ni kosa lisilosameheka.
Maadili ya kibinadamu yamejengwa juu ya heshima ya asili ya mwanadamu, Kila binadamu asiye na hatia bila kujali utaifa, dini au kabila, anastahiki maisha ya heshima, kuwanyima kwa makusudi watu chakula, maji na dawa ni jinai dhidi ya dhamira ya mwanadamu na ni kinyume na misingi ya kanuni ya kuishi kwa pamoja kibinadamu, tabia inayofanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya watu wa Ghaza si tu kwamba haina maadili wala ubinadamu, bali kwa mujibu wa nyaraka za kuaminika za sheria za kimataifa ni jinai ya kivita.
Tabia ya kikatili na isiyo ya kibinadamu inayofanywa na utawala wa Kizayuni ya kuzuia kuingia chakula na bidhaa muhimu kwa watu wa Ghaza ni ukiukaji wa wazi wa misingi ya kidini, kibinadamu, kimaadili na sheria za kimataifa, kitendo hiki si tu kwamba kinastahiki kulaaniwa duniani kote, bali pia kinastahiki kuchukuliwa hatua za kisheria na kuadhibiwa kimataifa, Kwa sasa ni wajibu kwa wanadamu wote
huru, mashirika ya haki za binadamu, taasisi za kidini na mataifa yote duniani, kutokaa kimya mbele ya jinai hii, bali kupaza sauti ya wanyonge wa Ghaza.
Mimi binafsi ninatoa pongezi kwa msimamo wenu kuhusu suala la Palestina, ambapo katika hotuba yako ya hivi karibuni, mlieleza wasiwasi wenu juu ya hali ya kutisha ya kibinadamu kwa watu wa Ghaza, na kuitaja hali hiyo kuwa mzigo wa uchungu mkubwa hasa kwa watoto, wazee na wagonjwa, kwa upande mwingine, mlitoa mwito kwa jamii ya kimataifa kuheshimu haki za kibinadamu za huruma, na kutekeleza wajibu wa kuwalinda raia, kuzuia adhabu za pamoja, matumizi kupita kiasi ya nguvu, na kuhamisha kwa lazima watu.
Mheshimiwa
Sasa kile kinachotokea Ghaza kwa hakika hakiwezi kufikirika kwa mujibu wa vigezo vyovyote vya kidini, kibinadamu au kimaadili, Kila siku watoto kadhaa wanapoteza maisha yao kwa sababu ya njaa na ukame; haya ni mauaji ya wazi wazi na huumiza moyo wa kila binadamu huru, katika hali hii ya kutisha, je, ikiwa Manabii wa Mwenyezi Mungu kama Nabii Musa (as), Nabii Isa (as), na Nabii Muhammad (saw) wangekuwepo, je, wangestahimili kuona mateso na msiba huu mkubwa? Au wangekuwa watazamaji tu wa matukio haya ya kikatili na yasiyo ya kibinadamu bila kutoa mwitikio wowote?
Inatarajiwa kuwa Mheshimiwa pamoja na viongozi wengine wa dini mtafanya juhudi madhubuti na zenye athari katika kuzuia jinai hizi dhidi ya ubinadamu zinazofanywa na utawala wa Kizayuni.
Mheshimiwa
Mwisho, napendekeza kuwa dini za Ibrahimu, sambamba na kulaani matumizi mabaya ya dini kwa ajili ya kutengeneza majanga yaliyotajwa hapo juu (mwendelezo wa miaka 80 ya jinai kwa kisingizio cha kuunda dola ya Kiyahudi kupitia kwa Wazayuni wahalifu), zifikirie kwa pamoja kuunda mfumo wa busara na wa kimataifa wa kutumia uwezo wao wote kwa ajili ya:
Kukataza na kulaani matumizi ya nguvu na ghasia, kwa upande mmoja
na kukuza amani na ubinadamu, kwa upande mwingine.
Hawza tukufu ya kielimu ya Qom
Hussein Nouri Hamedani
Maoni yako