Alhamisi 19 Juni 2025 - 18:43
Kuwavunjia heshima marajii kutasababisha hasira kwa umma wa kiisalamu

Hawza/ Mudiir wa hawza Qum ameeleza kuwa; Katika masiku ya karibuni viongozi wa mabeberu ulimwenguni na Mazayuni wamwaga damu, wameleta taharuki na hasira kwa waislamu baada ya kuwavunjia heshima Mraaji wa kiislamu hasa kiongozi wa mapinduzi ya Kiislamu.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, ujumbe wa Ayatollah Arafi katika kutete Marjaiyat ni kama ifuatvyo;

Kwa jina la Mwenyezimungu mwenye kuwavunja madhalimu na rehma na amani zimshukie mtume wake Pamoja na Ahli zake watoharifu.

Hivi sasa wakati wa kuamka na kusimama kidete na kwa msaada wa Mwenyezi Mungu Taifa la Irani na vijana shujaa na wenye ghera wa vikosi vya jeshi la Irani na makundi mengine yote ambyo yo yapo kwenye uga wa kuyalinda mapinduzi ya kiislamu, na Maraaji wote pamoja na hawza zote, zinaiunga mkono harakati hii ya kihistoria.

Hawza kwa kuanzishwa maraaji watuufu Pamoja na kutangaza kushikamana waislamu wote chini ya uongozi wa kiongozi mkuu wa mapinduzi ya kiislamu, na kukokoteza udharura wa kushikamana kama taifa moja, na kwa kukokoteza kuvikingia kifua vikosi vya jeshi la Irani, na vile vile udharura wa kuwa tayari watu wote na viongozi wote, na kuweka mazingira salama kwa ajili ya kuwatuliza wananchi, na kuendelea kuutetea utukufu wa taifa na Uislamu, Pamoja na kuwatetea Maraaji wa kishia, vyote hivi ni wadhifa wa kisheria kwa umma wa kiislamu na dola azote za kiislamu na ni nguzo asasi ya muqawama na wenye kutetea uhuru.

viongozi wa kibeberu ulimwenguni na Mazayuni wamwaga damu na wafuasi wa nyendendo za Hitla, wamewavunjia heshima Maraaji watukufu wa kishia na waislamu pia, Pamoja na kiongozi adhimu wa mapinduzi ya kiislamu mola amuhifadhi, na hili linahesabiwa kuwa ni jambo baya zaidi lililowahi kutokea katika karne zote, na ni lenye kufedhehesha na lenye kuleta hasira kwa Taifa la Irani na umma wa kiislamu kwa ujumla.

Kitendo hiki kichafu cha kuwatishia viongozi rasmi wa nchi ulimwenguni, hasa Marjaiyat tukufu ya kishia ni kinyume cha kanuni zote na misingi ya kimataifa, na tunaziomba taasisi zote za kimataifa za kielimu, kiutamaduni na nchi zote za kiislamu kuonesha misimamo yao juu ya hili na kuhakikisha kuwa kitendo hiki kichafu hakita jirudia tena, na vile vile tunaiomba serekali ya Irani Pamoja na mihimili yake yote mitatu kulifuatilia suala hili..

Hawza ya Qum na hawza nyengine Pamoja na walimu na shakhsia za kihawza na wanazuoni na maraaji watukufu, taasisi za kielimu na kiutamaduni, vyuo, pamona na watetezi wa haki za binadamu ulimwenguni kote, vyote hivi vinalizimika kusimama kidete juu ya kutetea shakhsia hii kubwa, na wafahamu kwamba kujikariri tena ujasiri kama huu kunaweza kupelekea maamuzi mengine yachukuliwe yatakayo sababisha hasira ulimwenguni na madhara yake si yenye kutabirika wala kutasawirika.

Na makafiri walipanga mipango na mwenyezi Mungu akapanga mipango, na Mwenyezi Mungu ndie mbora wa wenye kupanga.

Ali Reza Arafi

Mudiir wa hawza za Qum

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha