Kwa mujibu wa kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza Sheikh Ali Yasin katika hotuba yake msikitini katika Madrasa ya dini ya mji wa Sur alibainisha kwamba hati hiyo haitapitishwa, kwa sababu uamuzi upo mikononi mwa wananchi mashujaa, na siyo mikononi mwa maafisa wanaodai uongozi na uzalendo.
Sheikh Yasin alisisitiza: “Kumkabidhi mfungwa wa Kizayuni chini ya usimamizi wa Shirika la Msalaba Mwekundu bila ya masharti yoyote, kunafichua udhaifu wa watawala na kunazua alama kubwa za maswali.”
Akiuliza maswali muhimu, alisema: “Serikali inafanya nini kuhusu kuachiliwa wafungwa, angalau wale raia wasiokuwa na hatia, au kuhusu kubainisha hali zao? Kwa kuwa wao wanaishi chini ya hali za kifungwa za kigaidi za Kizayuni, na wamezuiwa kutembelewa na Shirika la Msalaba Mwekundu au taasisi yoyote ya kimataifa au ya kibinadamu.”
Rais wa Jumuiya ya Wanazuoni wa Sur alisisitiza kwamba Lebanon ni ya watu wake, si ya watawala wake, na kwamba matusi ya kimfumo ya kimadhehebu yanayoshuhudiwa siku hizi lazima yakome.
Akaongeza: “Watu wa kusini mwa Lebanon ndio wanaotoa funzo la uzalendo na uongozi, na si wale wanaolitumia vibaya taifa na maslahi yake huku wakidai uongozi na kutokuwa na upendeleo, ilhali wao hawakulinda misikiti wala makanisa dhidi ya uvamizi.”
Sheikh Yasin alisema: “Sisi tunaunga mkono mazungumzo ya kudumu, maisha ya pamoja na mwafaka wa kitaifa kutoka katika nafasi ya nguvu, haitakiwi kusikilizwa kauli za majivuno, hasa kutoka kwa sura fulani ambazo zinajua vyema kwamba wale waliolinda Baalbek dhidi ya kitisho cha makundi ya kigaidi ya kitakfiri, ndio hao hao waliolinda Arsal na Zahle wakati sura hizo zilipokuwa zikiangaika mbele ya wale waliowategemea.”
Sheikh Yasin alisema: “Baadhi ya maafisa wanayaona mapungufu ya uongozi ni kutokana tu na watu, silaha zao na jeshi ambalo lilikuwa huru na kulinda.”
Na mwishoni alisisitiza: “Palestina ni jambo la kibinadamu ambalo halina nafasi ya kutokuwa na msimamo, mradi wa ‘Israel Kubwa’ unapita mipaka ya sasa, hivyo basi, kusimama dhidi ya adui ni jukumu la kibinadamu, au kwa uchache la kitaifa, na kugeuka kinyume na jukumu hili kwa visingizio vya udanganyifu si chochote ila ni utekelezaji wa maagizo ya Marekani.”
Maoni yako