Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, msafara wa Nigeria unaoshiriki katika matembezi ya Arubaini ya Imam Husein (a.s.) kutoka Najafu hadi Karbala nchini Iraq, una uwepo wa kuvutia.
Msafara huu unasimamiwa na Dkt. Yushayub bin Sheikh, mwakilishi wa Sheikh Ibrahim Zakzaky.
Msafara huu utabaki Karbala hadi siku ya Arubaini, na ukiachilia mbali kumzuru Sayyid al-Shuhadaa (a.s.), pia utatoa huduma kwa mazuwari wengine wa Arubaini.
Chanzo: Tovuti rasmi ya Harakati ya Kiislamu ya Nigeria
Maoni yako