Jumanne 19 Agosti 2025 - 15:43
Maulidi ya Kitaifa Mwaka huu kufanyikia Mkoani Tanga

Hawza/ Maulidi ya kitaifa mwaka huu wa 2025 yamepangwa kufanyika Mkoani Tanga, katika wilaya ya Korogwe kwenye viwanja vya Shule ya Mazoezi Manundu

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Mufti na Shekh Mkuu wa Tanzania Dkt. Abubakar Zuber Bin Ally amekutana na Kamati ya Maandalizi ya Maulidi ya Kitaifa nyumbani kwake Korogwe kwa Mndolwa jana tareh 18 August ambapo kikao hicho kiliamua kwamba; safari hii Maulidi hayo yatafanyikia Mkoani Tanga Wilaya ya Korogwe.

Maulidi hayo ya Kitaifa ambayo hufanyika kila mwaka, mwaka huu yatafanyika tarehe 05-09-2025 katika Mkoa wa Tanga Wilaya ya Korogwe kwenye Viwanja vya Shule ya Mazoezi Manundu.

Katika Kamati hio alikuwepo Katibu Mkuu Bakwata Alhaj Nuhu Jabir Mruma, Muhammad Riyami Katibu wa Mkoa wa Tanga, Juma Mhina Katibu wa Wilaya ya Korogwe, Sheikh Said Ally Saleh Imam Mkuu wa Msikiti wa Ijumaa Tanga, Sharif Ally Saleh Msaidizi  wa Kadhi Mkoa Tanga na Sheikh Salim Bawazir.

Picha za baadhi ya wanakamati walio shiriki katika kikao hicho

Maulidi ya Kitaifa Mwaka huu kufanyikia Mkoani Tanga

Maulidi ya Kitaifa Mwaka huu kufanyikia Mkoani Tanga

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha