Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Habari la Hawza, kutoka Tehran, katika mkutano kati ya Muhammad Ali Amani, Katibu Mkuu wa Chama cha Mu’ātalafat - Islaam, na Muhammad Ibrahim al-Daylami, Balozi wa Jamhuri ya Yemen mjini Tehran, kulisisitizwa juu ya kuimarishwa kwa ushirikiano wa kistratejia na umoja wa umma wa Kiislamu mbele ya maadui wa pamoja.
Katika mkutano huu, Muhammad Ali Amani, Katibu Mkuu wa Chama cha Mu’ātalafah, kwa kulitukuza taifa la Yemen kutokana na mapambano yake ya kishujaa chini ya uongozi wa Ansarullah, alilitaja tukio hilo kuwa ni hamasa isiyo na mfano katika historia ya muqāwamah duniani.
Amani katika hotuba yake alieleza kuhusu nafasi ya msingi ya harakati ya Ansarullah kama uti wa mgongo wa mhimili wa muqāwamah katika ukanda, na akaongeza: Uthabiti na uvumilivu wa ndugu zetu Wayemeni mbele ya muungano wa wavamizi unaoongozwa na Marekani na utawala wa Kizayuni ni ukurasa wa dhahabu katika historia ya mapambano ya umma wa Kiislamu.
Aidha alitangaza utayari kamili wa Chama cha Mu’ātalafat - Islaam kusaini makubaliano ya ushirikiano wa pamoja na Ansarullah ya Yemen, na akasema: Makubaliano haya yanaweza kuwa chachu ya kuimarisha ushirikiano wa kistratejia katika nyanja za kisiasa, kitamaduni na kimedia baina ya pande mbili.
Kisha Muhammad Ibrahim al-Daylami, Balozi wa Yemen mjini Tehran, kwa kushukuru muqāwamah wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, alitoa pongezi kwa ushindi wa hivi karibuni wa Iran dhidi ya uvamizi wa utawala wa Kizayuni, na akaongeza: Ushindi huu, ingawa uliambatana na mashahidi wa thamani kubwa, lakini ulikuwa ushindi mkubwa kwa umma mzima wa Kiislamu na umechochea hamasa ya waumini.
Balozi wa Yemen mjini Tehran, kwa kueleza kuhusu msaada wa Yemen kwa Iran katika kipindi cha uvamizi wa hivi karibuni wa utawala wa Kizayuni, aliongeza: Jamhuri ya Yemen ilitangaza msaada wake wa kijeshi kwa Iran, kwa kuwa tunajua vyema ni huduma kubwa kiasi gani Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imezitoa kwa Uislamu na nchi za Kiarabu na Kiislamu.
Akieleza kuhusu nafasi ya uongozi wa busara wa Ayatollah Khamenei, alisisitiza: Ndugu zetu Wairani wanapaswa kufahamu kwamba wao wanailinda dunia nzima ya Kiislamu, na kushindwa kwao au ushindi wao ni sawa na kushindwa au ushindi wa Uislamu wote.
Al-Daylami, akikosoa kimya cha mashirika ya kimataifa mbele ya jinai za utawala wa Kizayuni, alibainisha: Njia pekee ya kuokoka ni umoja na kuimarisha nguvu za kijeshi na kiusalama, kama ambavyo Mwenyezi Mungu anavyosema katika Qur’ani Tukufu:
«وانزلنا الحدید»
Na tumeteremsha chuma,”
yaani Qur’ani tumeiteremsha kwa ajili ya mwongozo na chuma kwa ajili ya kukabiliana na maadui.
Balozi wa Yemen alikaribisha kuendelezwa kwa uhusiano wa kielimu na kitamaduni na Chama cha Mu’ātalafat-Islaam na akasema: Chama cha Mu’ātalafat kimejaa wasomi wabunifu na sisi tunakaribisha ushirikiano na chama hiki.
Al-Daylami akaongeza: Watu wa Iran ni watu wakubwa, na sehemu ndogo tu ya jamii ya wasomi wa kisiasa wanapaswa kuwa makini, Iran inastahiki kuonyesha ujumbe wa nguvu na ushindi wake na kuepuka kutuma ujumbe wa mgongano wa ndani na ujumbe wa udhaifu unaotoka kwa baadhi ya wasomi wa kisiasa, mkubwa zaidi anayefahamu ushindi wa Iran ni Israeli yenyewe na Marekani yenyewe.
Balozi wa Yemen, katika sehemu nyingine ya hotuba yake, alieleza kuhusu hatua kubwa zinazochukuliwa na Yemen kwa ajili ya kuwasaidia watu wanyonge wa Ghaza na akasema: Kila wiki tunafanya maandamano ya mamilioni nchini Yemen, na katika bunge na baraza la mawaziri, tumepitisha marufuku ya jumla ya bidhaa zote zinazohusiana na utawala wa Kizayuni na waungaji wake mkono wa Ulaya.
Alitoa taarifa pia kuhusu kuundwa kwa kikosi cha Basiji cha watu milioni moja nchini Yemen, na akaongeza: Kikosi hiki mbali na jeshi na makundi ya kijihadi, tunatarajia tajiriba hii itajikariri katika nchi za Kiarabu ambazo bado zimo katika usingizi.
Balozi wa Yemen katika kusisitiza juu ya umoja wa uwanja wa muqāwamah, alibainisha: Tangu siku za mwanzo, tumelifanya jambo la umoja wa uwanja wa muqāwamah kuwa kaulimbiu ya kazi yetu, na tunaamini kwamba Iraq, Yemen, Lebanon, Palestina na Iran vyote ni viwanja vya pamoja vinavyopaswa kuimarishwa kwa kuongezwa viwanja vipya.
Mwishoni, Katibu Mkuu wa Chama cha Mu’ātalafat-Islaam, akieleza nukuu ya Kauli ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ambaye amesema: “Yemen yenye ujasiri ni mti imara mbele ya dhoruba kali za mabeberu wa dunia”, alisisitiza juu ya ulazima wa mshikamano na umoja wa umma wa Kiislamu kwa ajili ya kukabiliana na njama za adui.
Mwisho wa taarifa
Maoni yako