Jumanne 26 Agosti 2025 - 16:12
Jopo la Wanazuoni wa Kiislamu Lebanon: Muda wa kuwa Ardhi zilizokaliwa kimabavu hazijakombolewa na uvamizi haujakoma, silaha za muqawama haziwezi kujadiliwa

Hawza/ Jopo la Wanazuoni wa Kiislamu wa Lebanon limesema: Serikali ya Lebanon inaendelea kung’ang’ania, kuendeleza maneno ya kisiasa yenye uchochezi na vitisho visivyo na maana kuhusiana na suala la silaha za muqawama

Kwa mujibu wa ripoti ya Idara ya tarjuma ya Shirika la Habari la Hawza, Baraza la Utendaji la Jopo la Wanazuoni wa Kiislamu wa Lebanon limefanya kikao chake cha kawaida na kujadili matukio mapya ya Lebanon na Palestina, taarifa iliyotolewa imebainisha kwamba: Serikali ya Lebanon bado inang’ang’ania, kuongeza shutuma na vitisho visivyo na msingi kuhusiana na silaha za muqawama, kwa kuthibitisha hili, jana ilifanyika maigizo ya kichekesho kuhusu kile walichokiita kukabidhi silaha za kambi.

Jopo hilo limeongeza kuwa: Imebainika kuwa jambo hili lilikuwa makubaliano ya siri kati ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina na serikali ya Lebanon kwa ajili ya kukabidhi chuma chakavu kilichosafirishwa kwa gari ndogo ya kiraia iliyokodiwa, makundi ya muqawama wa Kipalestina yameeleza wazi kwamba hakuna kitu kinachoitwa kukabidhi silaha, na kwamba silaha za kambi zimefungamana na haki ya kurejea, na muda wa kuwa wakimbizi wote wa Kipalestina hawajarudi katika nchi zao, silaha hazitakabidhiwa.

Jumuiya ya wanazuoni imeendelea kusema: Suala la silaha za muqawama wa Lebanon ni suala nyeti ambalo linapaswa kushughulikiwa kwa mujibu wa maslahi ya kitaifa ya juu yanayohakikisha uhuru, mamlaka na uhuru wa Lebanon kupitia kuzikomboa ardhi zote zilizokaliwa kwa mabavu, kusitisha uvamizi wa utawala wa Kizayuni na kuwarejesha mateka, bila shaka, iwapo silaha zitakabidhiwa, jambo hili halitatimia.

Jumuiya ya Wanazuoni wa Lebanon imesema: Inatarajiwa kwamba maeneo yaliyokaliwa na adui Mzayuni yataongezeka, kwa kuwa adui huyu kupitia baadhi ya viongozi wake anatishia kutaka kuyakalia kimabavu maeneo mapya kusini mwa Lebanon na kufikia umbali mkubwa zaidi ya ule alioukalia kabla ya mwaka 2000.

Jumuiya hiyo ikaendelea kusema: Hivyo basi, serikali ya Lebanon inapaswa kusitisha maamuzi yake yanayohusiana na karatasi ya Marekani na kuizingatia kana kwamba haijawahi kuwepo, mpaka pale kuondoka kwa adui Mzayuni katika ardhi zilizokaliwa kutakapofanikishwa, uvamizi wa anga, nchi kavu na baharini utakapositishwa na mateka watakaporejeshwa, hapo ndipo inaweza kujadiliwa namna ya kunufaika na silaha za muqawama ndani ya mfumo wa ulinzi wa taifa.

Jumuiya ya wanazuoni imeashiria kuwa: Kwa upande mwingine, Walebanon wameshangazwa na uamuzi wa kumkabidhi raia wa Kizayuni kwa utawala wa Kizayuni, baada ya karibu mwaka mmoja wa kutiwa nguvuni na usalama wa umma, jambo hili limeibua maswali kwamba vipi inawezekana kumkabidhi raia wa Kizayuni bila kupata fidia yoyote, ilhali tunao raia kumi na tisa wa Lebanon walioko kifungoni kwa adui Mzayuni? Kwa nini hakukuwa na mazungumzo ya kubadilishana mateka kwa ajili ya kuwaachia huru mateka wetu? Je, serikali ya Lebanon kama kawaida imetekeleza amri ya Marekani kwa ajili ya kumwachia huru?

Jumuiya hiyo imelaani kitendo cha serikali ya Lebanon kumkabidhi raia wa Kizayuni kwa utawala wa Kizayuni bila kumjumuisha kwenye mchakato wa kubadilishana wafungwa na raia kumi na tisa wa Lebanon walioko mikononi mwa adui Mzayuni, na ikataka kufanyike uchunguzi wa kina juu ya ni nani aliyeamua kumwachia huru, kwani hii ni khiyana kubwa ambayo wote waliohusika wanapaswa kuwajibishwa.

Jumuiya ya Wanazuoni wa Kiislamu, imeonesha ridhaa yake juu ya yale yaliyoelezwa na uongozi wa jeshi; kwamba kwa nguzo za serikali na Hizbullah limefahamishwa kwamba, jeshi halitachukua hatua yoyote itakayodhoofisha uthabiti wa ndani na halitaruhusu upande wowote kutumia mivutano iliyopo ili kuanzisha mgongano kati ya jeshi na muqawama.

Jumuiya hiyo imeongeza: Kauli hizi zinaonesha weledi na busara kwenye uongozi wa jeshi katika kushughulikia suala nyeti la kiwango hiki, na hamu yake ya kuhifadhi amani ya ndani na kuliweka taifa mbali na hatari za vurugu za kiusalama.

Jopo la wanazuoni pia limelaani ukiukaji endelevu wa azimio 1701, na azimio la kusitisha mapigano na adui Mzayuni kwa kulenga nyumba ya mbao mjini Maroun al-Ras usiku wa jana, sambamba na ukiukaji wa kila siku, mashambulizi ya mfululizo ya mizinga dhidi ya maeneo yaliyopo mstari wa mbele, na uvamizi wa mara kwa mara kwenye ardhi ya Lebanon kwa lengo la kupanua maeneo yake yaliyokaliwa katika maeneo matano yaliyotajwa.

Jumuiya hiyo imetoa heshima kwa muqawama wa Ghaza kwa ajili ya operesheni zao za kifahari dhidi ya wanajeshi wavamizi wa Kizayuni, kwa shambulizi lililofanywa na wapiganaji wa muqawama wapatao ishirini waliokuwepo katika kambi ya wavamizi huko Khan Yunis kusini mwa Ukanda wa Ghaza, kurusha makombora ya kupambana na vifaru katika kambi hiyo na kumpiga risasi kwa umakini kamanda wa tanki la Merkava na kumsababishia jeraha hatari lililopelekea kufa kwake.

Jumuiya ya wanazuoni mwishoni imesema: Jambo hili linathibitisha kwamba muqawama bado una maandalizi imara na uko tayari kuendeleza na kupanua operesheni zake, ikiwa adui Mzayuni atataka kuivamia Ghaza, kama anavyodai, vikosi vinavyo hitajia shahada vitakuwa macho dhidi yake.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha