Alhamisi 4 Septemba 2025 - 18:43
Ujumbe wa rambirambi kutoka kwa Ayatollah A‘rafi kuwaelekea wananchi wa Afghanistan

Hawza/ Hawza za Kielimu za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, kwa mujibu wa majukumu na risala zake za kidini na kibinadamu, ziko tayari kutoa kila aina ya msaada na ushirikiano kwenye kutatua matatizo na kupunguza machungu kwa waliothirika kutokana na tetemeko la ardhi la kusikitisha nchini Afghanistan

Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Habari la Hawza, matini ya ujumbe wa rambirambi kutoka kwa Ayatollah A‘rafi kuwaelekea wananchi wa Afghanistan kufuatia kutokea kwa tetemeko la ardhi la kusikitisha nchini humo ni kama ifuatavyo:

Bismillahi Rahmani Rahim

Inna lillahi wa inna ilayhi raji‘un

Kufuatia kutokea tetemeko la ardhi la kusikitisha nchini Afghanistan ambalo limepoteza maisha ya idadi kubwa ya wananchi wapendwa wa nchi hiyo, mioyo yetu imejaa huzuni kubwa.

Msiba huu mkubwa nauwasilisha kwa wananchi jasiri na wavumilivu wa Afghanistan, hususan kwa maulamaa na shakhsia kubwa za kidini na kitamaduni, pamoja na wafiwa waliopata msiba na familia za wahanga, rambirambi na ta‘ziyah zetu.

Hawza za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, kwa mujibu wa majukumu na risala zake za kidini na kibinadamu, ziko tayari kutoa kila aina ya msaada na ushirikiano katika muelekeo wa kutatua matatizo na kupunguza machungu ya waathirika.

Ali Reza A‘rafi
Mkurugenzi wa Hawza za Kielimu Iran

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha