Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Maullidi ya Mtume Muhammad (saw) kwa mwaka huu wa 2025 yamepangwa kufanyika siku ya jumatano tareh 10/9/2025 kuanzia saa 8:00 pm katika viwanja vya Pipo jijini Daresalam.
Kama ilivyo ada maulidi hayo hufanyika kila mwaka chini ya usimamizi wa Samaaht Sheikh Jalala Hemedi Mudiri wa Hawza ya Imam Sw'adiq (as) na Sheikh mkuu wa Jumuiya ya Tanzania Ithnaasharia Community, mwaka huu maulidi hayo yamepangwa kufanyika huku mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mh. Jakaya Mrisho Kikwete, Raisi mstaafu wa awamu ya nne wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzani. Hawza ya Imaam Swaadiq (as) ikishirikiana na Jumuiya ya Tanzania Ithnaasharia Community (TIC), inawaalika waumini wote duniani kushiriki katika hafla hiyo pendwa kwa ajili ya kukumbuka mazazi ya Mtume Muhammad (saw).
Maoni yako