Kwa mujibu wa taarifa ya Idara ya tarjuma ya Shirika la Habari la Hawza, siku ya Jumatatu kikao cha hadhara kiliitishwa na Waislamu wa Stittsville katika mji huo, kikao hiki kilifanyika baada ya waharibifu kuchora picha za kibaguzi na za kupinga Uislamu juu ya jengo la jumuiya hiyo.
Mheshimiwa Amir Siddiqui, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Waislamu wa Stittsville, alisema: “Tukio hili ni moja tu kati ya matukio machungu ambayo jamii ya Waislamu wa Kanada inakabiliana nayo kutokana na propaganda za chuki dhidi ya Uislamu, tunataka kuchukuliwe hatua madhubuti kutoka katika ngazi zote za serikali ya Kanada.”
Akaongeza: “Tukio hili ni dhidi ya watu wote wa Kanada, siyo tu dhidi ya jamii ya Waislamu.”
Baada ya tukio hili, Meya wa Ottawa alitangaza kuwa yupo katika maandalizi ya kikao kwa ajili ya viongozi wa kidini wa nchi hii ili kupata suluhisho mwafaka la janga hili, katika kikao hicho alisisitiza: “Tunatumai matukio ya aina hii yatapungua.”
Chanzo: Yahoo News
Maoni yako