Kwa mujibu wa taarifa ya Idara ya tarjuma ya Shirika la Habari la Hawza, moja ya vikundi vya ukombozi wa Palestina katika tamko lililochapishwa na vyombo vya habari vya Quds Press limesema: Leo dunia inashuhudia mauaji ya wanawake na watoto na kutiririka mito ya damu Palestina, pamoja na hayo kimya cha aibu kimechukua nafasi kiasi kwamba inaonekana kana kwamba imeshirikiana na wauaji.
Katika kuendelea kwa tamko hilo imesemwa: Hasa mjini Ghaza kunashuhudiwa hatua ya kikatili zaidi ya mauaji ya watu; hakuna mahali salama Ghaza, na huduma za kitabibu zimepungua kwa kiwango kikubwa mno huku vifaa vya matibabu vikikaribia kuwa sifuri.
Ziara ya balozi wa Marekani nchini Israel na uchochezi wa kuiteka Bethlehemu na sehemu nyingine za Palestina ni dalili ya ushiriki na athari ya moja kwa moja ya Marekani katika vita na mauaji ya kimbari Ghaza.
Mwishoni mwa tamko hilo imesemwa: Tunataka kuongezwa shinikizo la wananchi na kisiasa dhidi ya serikali ya Marekani, kwani kwa kufanya hivyo tutaweza kusimamisha vita na njaa.
Chanzo: MIDDLE EAST MONITOR
Maoni yako